WANAFUNZI ZAIDI YA 700 KUTUMIA MABWENI YALIYOBARABATIWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NOVEMBA

Published on Saturday 21 September, 2019 19:10:44

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema mabweni mawili ya wanafunzi maarufu “hall 5 na hall 2 “katika Chuo kikuu cha Dar es salaam yaliyokarabatiwa yatachukua wanafunzi 788 . Ndalichako amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa Mabweni, Vyumba vya mihadhara na Ofisi katika Ndaki ya Uhandisi Katika Chuo hicho.

Mabweni hayo, yanakarabatiwa na Serikali kwa Shilingi za Tanzania zaidi ya Bilioni 4.5, ukarabati ukihusisha kuweka upya mifumo ya maji safi na taka, mifumo ya umeme, kuwekwa upya makabati na milango mipya, madirisha uwekaji vigae vipya vya ukutani na uwekaji “lift” mpya.

Ukarabati huu unatarajiwa kukamilika, ifikapo mwezi Oktoba, 2019. unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT- na kusimamiwa na kurugenzi ya milki ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ulianza 2018. Mabweni haya yalijengwa mwaka 1965 na kwa mara ya kwanza yanafanyiwa ukarabati mkubwa baada ya kusitisha utumiaji kutokana na uchakavu.

Waziri Ndalichako amepongeza kasi na ubora wa kazi ya ukarabati huo, huku akipongeza hatua ya chuo Kikuu kutumia wataalamu wake wa ndani kusimamia kazi za ukarabati katika chuo hicho.

“nimefurahishwa na kazi hii ni bora na kasi ya kazi ya ukarabatiwa mabweni haya kwani yataongeza uwezo wa chuo kutoa huduma ya Malazi kwa wanachuo zaidi ya 11,100. Naagiza uongozi mko hapa maagizo kwa hakikisheni ukarabati wa mabweni haya na majengo katika Ndaki ya Uhandisi unakamilika kabla ya kufunguliwa Chuo Novemba ili isiwe bugudha kwa wanafunzi, Mwaka huu ”

Akimkaribisha Waziri wa Elimu, Makamu Mkuu wa Chuo Cha Dar es salaam Profesa Wiliam Anangisye ameishukuru Serikali ya awamu ya tano na Waziri wa Elimu kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya kuboresha ili ili kuhahakikisha vijana wanapata elimu katika mazingira bora. Amemuhakikishia Waziri Ndalichako kuwa Chuo kitasimamia na kuhakikisha kazi zinazoendelea zinakamilika kwa wakati .

“ tunaishuruku serikali ya Awamu ya Tano na wewe Mheshimiwa kwani maendeleo haya ni maono ya Serikali na yanatekelezwa na serikali , nasi tunakuhakikishia pia kuendelea kutunza miundo mbinu hii na kutumia mapato ya ndani kuyaendeleza”

Nae Dr liberato Haule Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Maendeleo akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi amezungumzia ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi kuwa umefikia asilimia 45 na kuwa utagharimu shilingi bilioni 1.5 .

“ napenda kutoa taarifa kuwa mradi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya Uhandisi unahusisha majengo ya ofisi na madarasa, nyumba za wafanyakazi na bweni moja lililopo kitalu G. nikuhahakikishie Mh Waziri kuwa mataraji yetu ni kuwa kazi itakamilika kwa wakati uliopangwa Novemba mwaka huu“

Nae Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bi. Jackline Ndombele, ameishukuru serikali kwa ukarabati mkubwa unaoendelea hall 5 na hall 2 na kwamba utasaidia sana kuongeza idadi ya wanafunzi wanaokaa chuo, kwani kwa sasa wengi wanakaa nje ya Chuo.

Read 2157 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022