WANAFUNZI TANZANIA NA CHINA KUBALISHANA UZOEZI

Published on Thursday 01 December, 2022 16:30:22

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameshuhudia utiaji  saini wa makubaliano ya ushirikiano  kati ya Taasisi  ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) na Taasisi ya Ufundi ya  Chonqing (CQVIE) kutoka nchini China.

Waziri Mkenda amesema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka Tanzania ikiwa katika mchakato wa MAGEUZI makubwa katika elimu.

Miongoni mwa makubaliano ya ushirikiano  baina ya Taasisi hizo ni kubadilishana Wanafunzi na Walimu (exchange program ) ili kubadilishana uzoefu katika ujuzi wanaopata katika mafunzo.

Pia wanafunzi wanufaika wa programu hiyo watakuwa na sifa za kufanya kazi katika makampuni mbalimbali nchini China.

Prof. Mkenda amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha ushiriano huo unadumu na unakuwa endelevu kwa maslahi ya nchi hizo mbili.

Read 860 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 216 0270               
  •                +255 737 962 965
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top