WANAFUNZI SUA KUFANYA KILIMO CHA BIASHARA

Published on Tuesday 28 June, 2022 10:54:46

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo wameunda kikundi cha umoja wa SAEG (Sokoine Agri-Enterprise Group) kwa lengo la kufanya kilimo biashara ili kujiongozea kipato wanapokuwa chuoni hapo kwa kutumia nguvu zao wenyewe.

Akizungumza na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko siku ya Jumatatu tarehe 27 Juni 2022, Bw. Gregory Pankas wa mwaka wa kwanza kutoka kozi ya Sayansi ya Udongo na Mazao amesema kuwa kwa sasa wamefanikiwa kulima kiasi cha nusu heka ya Alizeti, nusu heka ya nyanya pamoja na mboga mbalimbali kwenye mashamba ya SUA.

Alisema wamekuwa wakitumia muda wao wa ziada kuingia shambani na kufanya kazi za uzalishaji. 

“Kutokana na soko la Alizeti kuwa adimu tumeamua kulima Alizeti kwa lengo la kujifunza lakini pia kama fursa ya kibiashara sokoni ili kuisaidia jamii kuondokana na uhaba wa mafuta ya Alizeti”, alisema Bw. Gregory. 

Pamoja na changamoto ya hali ya hewa vijana hao hawakukata tamaa na waliamua kutumia maji kutoka mto Ngerengere unaopita karibu na mashamba hayo ili kuweza kumwagilia mazao yao. Baadhi ya mazao kama nyanya na mboga tayari wameanza kuvunwa na kupelekwa sokoni.

Read 349 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022