Uhamisho wa mwanafunzi kwa shule za msingi

Published on Friday 04 March, 2016 22:31:49

[accordion] [acc_item title="Taratibu za uhamisho wa mwanafunzi wa elimu ya msingi anayehamia nje ya nchi"]

a.) Mzazi/ Mlezi aandike barua kwenda katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (WEST) akifafanua ombi lake kwa kutoa sababu za msingi kuhusu uhamisho huo. Barua hiyo iwe ni ya kupitia kwa mwalimu mkuu, Afisa Elimu wilaya na Afisa Elimu wa mkoa husika.

b). Vitambulisho vya barua viwe:-

  1. Kadi ya Maendeleo ya mwanafunzi wa Elimu ya Msingi anaeingia Nchini.
  2. Barua iwe na picha ya mwanafunzi

c). Afisa wa Wizara anayehusika atamwandikia barua ya kumtambulisha nchi anakokwenda.

[/acc_item] [acc_item title="Taratibu za uhamisho wa mwanafunzi wa Elimu ya Msingi anayeingia Nchini"]

a). Mwanafunzi atapokelewa na WEST kwa kuonesha barua toka Wizara ya nchi anakotoka, barua hiyo isainiwe na kuwekwa muhuri na mamlaka husika.

b). Vitambulisho vya barua

  1. Taarifa ya maendeleo ya mwanafunzi kuishia darasa alilopo.
  2. Vivuli vya passport ya mwanafunzi na mzazi/mlezi.
  3. Taarifa ya usajili wa mwanafunzi
  4. Kibali cha ukazi wa mwanafunzi kuonyesha muda atakaokuwepo nchini
  5. Picha za passport 4
  6. Ni vizuri mwanafunzi akabeba daftari za masomo alizotumia hivi karibuni maana zinaweza kuhitajika.

c). Afisa wa Wizara anayehusika atamjazia fomu mzazi/mlezi za kumtambulisha mwanafunzi kwa mamlaka husika.

[/acc_item] [/accordion]

NUKUU: Utaratibu huu ni kwa shule za Serikali na zisizo za Serikali.

Read 31950 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 216 0270               
  •                +255 737 962 965
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Kituo cha Huduma kwa Mteja