TUNAELEKEA KUFANYA MAGEUZI KATIKA ELIMU, MAGEUZI YAANZIE KWENYE UTENDAJI WETU.

Published on Tuesday 28 February, 2023 10:00:03

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa umahiri, weledi na ubunifu ili malengo ya sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaweze kufikiwa.

Prof. Nombo ametoa wito huo jijini Dodoma wakati wa mapokezi yake na Naibu Katibu  Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema Wizara hiyo imepewa majukumu makubwa ya kuhakikisha elimu inayotolewa kwa Watanzania inakuwa bora na kuimarisha Sekta ya Sayansi na Teknolojia.

Ameongeza hivi sasa Wizara ipo katika hatua za mwisho za kuhuisha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na Mitaala, huku akisisitiza kuwa si Tanzania pekee inayofanya mageuzi hayo bali Dunia nzima ipo katika kufanya mageuzi ya elimu.

"Mageuzi katika utendaji kwa kufanya kazi kwa weledi,  umahiri,  ubunifu na uwazi  ni muhimu ili kufikia yale mageuzi tunayoyatamani katika sekta ya elimu," amesisitiza Katibu Mkuu.

Prof. Nombo amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaamini na kumpa nafasi katika utumishi huo.

Aidha amewashukuru Makatibu Wakuu waliotangulia kwa kuweka misingi imara katika kuelekea mageuzi nchini.

Naye Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Franklin Rwezimula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kutumikia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi ili kuendelea kuboresha sekta ya elimu.
[28/02, 15:00] Ipyana: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) inaendesha mafunzo ya siku tano kwa walimu wa shule za sekondari za umma wanaofundisha masomo ya Sayansi na Hisabati.

Katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Mradi unatarajia kutoa mafunzo kwa walimu 20,000 wa Sayansi na Hisabati na utaendelea kutoa mafunzo haya katika mwaka ujao wa fedha ili kukamilisha kutoa mafunzo kwa walimu wote wa shule za sekondari za umma wanaofundisha  masomo ya Sayansi na Hisabati.

Mpaka sasa mafunzo hayo yameshatolewa kwa zaidi ya walimu 8,000 kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Morogoro, Pwani, Dodoma, Singida na Tabora.

Read 345 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 216 0270               
  •                +255 737 962 965
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Kituo cha Huduma kwa Mteja