Rais wa Skauti Tanzania Prof. Adolf Mkenda ametangaza tarehe rasmi ya kufanyika Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti nchini.
Tarehe hiyo imetangazwa leo Juni 3, 2022 na Rais huyo ambae pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokutana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Lela Muhamed Musa katika kikao cha mashauriano juu ya Mkutano huo ambapo amesema utafanyika Julai 2, 2022 jijini Dodoma.
Mkenda amesema pamoja na kuwa agenda kuu ya Mkutano huo ni Uchaguzi lakini pia kutakuwa na majadiliano mengine kuhusu chama hicho. Aidha ameongeza kuwa Mawaziri hao wawili wataunda kamati itakayoratibu namna kuboresha utekelezaji wa majukumu ya Skauti Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe. Lela Musa amemshukuru Prof. Mkenda kwa kikao hicho cha mashauriano na Kusisitiza juu ya wajumbe kuanza kujiandaa kushiriki ikiwa ni pamoja na wagombea.
Ameongeza kuwa katika mkutano huo pia kutajadiliwa juu ya Ushiriki wa Zanzibar katika masuala ya Skauti ili iwekwe sawa katika katiba ya sasa ya Chama hicho.
" Kubwa zaidi nawataka Skauti wote kusimama imara, kurejesha Umoja na kulinda heshima kwa kuwa Skauti ni heshima, maadili na uzalendo. Hii itasaidia kuendeleza sifa nzuri ya Skauti Nchi na Kimataifa", amesema Mhe. Lela Musa.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Ali Abdul Gulam Hussein, Mmoja wa wadhamini Wakuu Mhasham Askofu Gervas John Nyaisonga, Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Khamis Juma, Kamisha wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa na Kamisha Mkuu Mtendaji wa Skauti Bibi. Kitali