Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, inawatangazia Wakuu wote wa Shule za Msingi na Sekondari kuhusu kuwepo kwa Shindano la Insha la Jumuiya ya Madola la mwaka 2020. Shindano hili ni kwa ajili ya vijana wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18. Mada ya mwaka huu ni “Climate Action in the Commonwealth” Mwisho wa shindano ni tarehe 30 Juni, 2020.
Washiriki wajisajili na kufuata maelekezo kupitia tovuti ya www.theres.org/competition.