1. UTANGULIZI
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Sekondari. Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha SITA wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
2. SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02) za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari Kidato cha I-IV. Aidha, kwa waombaji ambao moja ya “Principal Pass”mbili ni somo la Uchumi “Economics”, wanaweza kuomba kozi za fani ambazo ni Michezo (Physical Education and sports), Muziki, Sanaa za Ufundi (Fine Arts), na Sanaa za Maonesho (Theatre and Performing Arts).
3. AINA ZA MAFUNZO
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo
Na. |
AINA YA MAFUNZO |
SIFA ZA KUJIUNGA |
CHUO |
MUDA WA MAFUNZO |
1 |
Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati |
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili katika masomo ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA kwa kuzingatia Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari. Masomo hayo ni: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agriculture Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science. |
Mamire TC, Monduli TC, Mandaka TC, Butimba TC, Klerruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC na Tabora TC |
Miaka 2
|
2 |
Stashahada ya Sayansi ya Jamii, Biashara na Lugha |
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili katika masomo ya sanaa yanayofundishwa katika shule za Sekondari Kidato cha I-IV. Masomo ya sanaa yanayofundishwa katika shule za Sekondari kidato cha I-IV ni : Kiswahili, English, History, Geography, Civics, Commerce na Book keeping. |
Bunda TC, Mtwara (K) TC, Marangu TC, Nachingwea TC, Shinyanga TC, Mandaka TC, Mpuguso TC, Dakawa TC, Butimba TC, Tabora TC, Morogoro TC, Tarime TC, Shinyanga TC, Bunda TC
|
Miaka 2
|
3 |
Stashahada ya Ualimu Michezo, Muziki, Sanaa za Ufundi na Sanaa za Maonesho |
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili kama kama ilivyoainishwa hapa chini kwa kila kozi:
|
Butimba TC |
Miaka 2
|
(a) Sanaa za Ufundi: masomo ya Fine Arts, Basic Mathematics, Chemistry, History, Physics, English na Civil Engineering. |
Butimba TC |
Miaka 2
|
||
(b) Sanaa za Maonesho: masomo ya English, Literature in English, Kiswahili, Geography na History. |
Butimba TC |
Miaka 2
|
||
(c) Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na masomo ya English, Kiswahili, Physics, Geography, History na Biology. |
Butimba TC |
Miaka 2
|
||
(d) Elimu kwa Michezo: masomo ya Physical Education and sports, Languages, na Biology. |
Butimba TC, Mpwapwa TC na Mtwara (K) |
Miaka 2
|
B. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI)
Na. |
AINA YA MAFUNZO |
SIFA ZA KUJIUNGA |
CHUO |
MUDA WA MAFUNZO |
|
1 |
Stashahada ya Elimu Maalum (Mafunzo Kazini) Sekondari |
Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada au Shahada na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka 2; Aidha awe aliyefaulu masomo ya Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Sita |
Patandi TC |
Miaka 2 |
Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.