UTANGULIZI
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (Sayansi miaka mitatu). Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha NNE wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (sayansi miaka mitatu) ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III.
AINA YA MAFUNZO NA SIFA
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.
Na. |
AINA YA MAFUNZO |
SIFA ZA KUJIUNGA |
VYUO |
MUDA WA MAFUNZO |
|
1 |
Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi |
(a) Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati,English na Sayansi.
(b) Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.
|
Bustani TC, Ilonga TC, Kabanga TC, Katoke TC Kitangali TC, Kinampanda TC, Mandaka TC Mtwara (U) TC, Mhonda TC, Murutunguru TC Mpuguso TC, Singachini TC, Tandala TC, Tarime TC Vikindu TC, Nachingwea TC, Ndala TC, Mamire TC, Shinyanga TC, Marangu TC,Tabora TC, MonduliTC, Sumbawanga TC na Dakawa TC |
Miaka 2 |
|
2 |
Astashahada ya Ualimu Elimu Maalum |
(a) Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati na Sayansi
(b) Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.
|
Patandi TC, Kabanga TC na Mpwapwa TC |
Miaka 2 |
|
3 |
Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali |
(a) Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati na Englsh.
(b) Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza. |
Kinampanda TC, Nachingwea TC, Mhonda TC Tarime TC, Vikindu TC, Mpuguso TC, Mandaka TC, Singachini TC Murutunguru TC, Kabanga TC, Bustani TC Ndala TC, Katoke TC, Bunda TC, Tarime TC, Sumbawanga TC, Tabora TC |
Miaka 2
|
|
4 |
Astashahada ya Ualimu Elimu kwa Michezo |
(a) Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya sayansi na hisabati.
(b) Aliyehitimu Kidato cha VI au uzoefu katika michezo ni sifa ya nyongeza. |
Tarime TC, Mtwara (K) TC, Ilonga TC, Tabora TC |
Miaka 2
|
|
5 |
Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (English Medium) |
(a) Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu somo la English
(b) Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza. |
Dakawa TC, Marangu TC, Tabora TC
|
Miaka 2
|
|
1 |
Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati |
Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III kwa masomo ya: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agriculture Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science, Commerct, Accountant. |
Monduli TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC na Tabora TC na Mandaka TC na Sinyanga TC |
Miaka 3
|
|
Na. |
AINA YA MAFUNZO |
SIFA ZA KUJIUNGA |
CHUO |
MUDA WA MAFUNZO |
|
|
|
||||
1 |
Astashahada Elimu Maalum (Mafunzo kazini) Msingi |
Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Astashahada, Stashahada au Shahada kwa ufaulu wa angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Nne na awe na uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka miwili (2) |
Patandi TC |
Miaka 2 |