TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA ASTASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI, MSINGI NA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU SEKONDARI (SAYANSI MIAKA MITATU) KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Published on Tuesday 17 May, 2022 13:26:40

UTANGULIZI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (Sayansi miaka mitatu). Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha NNE wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (sayansi miaka mitatu) ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III.

AINA YA MAFUNZO NA SIFA

Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo

 1. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA ASTASHAHADA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

Na.

AINA YA MAFUNZO

SIFA ZA KUJIUNGA

VYUO

MUDA WA MAFUNZO

1

 

 

 

 

Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi

(a)      Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati,English na Sayansi.

 

(b)      Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

 

 

Bustani TC, Ilonga TC, Kabanga TC, Katoke TC

Kitangali TC, Kinampanda TC, Mandaka TC

Mtwara (U) TC, Mhonda TC, Murutunguru TC

Mpuguso TC, Singachini TC,

Tandala TC, Tarime TC Vikindu TC, Nachingwea TC, Ndala TC, Mamire TC, Shinyanga TC, Marangu TC,Tabora TC, MonduliTC, Sumbawanga TC na Dakawa TC

 

 

 

 

Miaka 2

2

 

 

 

Astashahada  ya Ualimu Elimu Maalum

(a)      Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati na Sayansi

 

(b)      Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

 

Patandi TC,

Kabanga TC na Mpwapwa TC

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 

 

3

 

 

 

Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali

(a)      Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III   Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati na Englsh.

 

(b)      Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

Kinampanda TC, Nachingwea TC, Mhonda TC

Tarime TC, Vikindu TC, Mpuguso TC, Mandaka TC, Singachini TC

Murutunguru TC, Kabanga TC, Bustani TC

Ndala TC, Katoke TC, Bunda TC, Tarime TC, Sumbawanga TC, Tabora TC

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 

 

4

 

 

 

Astashahada ya Ualimu Elimu kwa Michezo 

(a)    Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya sayansi na hisabati.

 

(b)    Aliyehitimu Kidato cha VI au uzoefu katika michezo ni sifa ya nyongeza.                               

 

 

Tarime TC, Mtwara (K) TC, Ilonga TC, Tabora TC

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 

 

5

Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (English Medium)

(a)  Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu somo la English

 

(b)    Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.                               

 

Dakawa TC, Marangu TC, Tabora TC

 

 

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 

 1. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI (SAYANSI NA BIASHARA)

 

1

 

Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati

 

Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III  kwa masomo ya: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agriculture Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science, Commerct, Accountant.

 

Monduli TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC na Tabora TC na Mandaka TC  na Sinyanga TC

 

 

 

 

 

Miaka 3

 

                  

 1. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (ASTASHAHADA ELIMU MSINGI ELIMU MAALUMU)

 

 

Na.

AINA YA MAFUNZO

SIFA ZA KUJIUNGA

CHUO

MUDA WA MAFUNZO

 

 

1

Astashahada Elimu Maalum (Mafunzo kazini) Msingi

Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Astashahada, Stashahada au Shahada kwa ufaulu wa angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Nne na awe na uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka miwili (2)

Patandi TC

Miaka 2

 

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

 • Wahitimu wa kidato cha nne waliohitimu kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 wanaruhusiwa kutuma maombi.
 • Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kielektroniki kupitia tovuti (tcm.moe.go.tz)
 • Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki.
 • Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi.
 • Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada au Shahada.
 • Walimu Kazini watapaswa kuambatisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao;
 • Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia 07/06/2022) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.
 • Barua na fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
 • Mwisho wa kutuma maombi kwa Mafunzo ya Ualimu ni tarehe 31/05/2022.   

            Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.

PAKUA FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA KWA KILA CHUO HAPA CHINI.

{jd_file file==229}

{jd_file file==230}

{jd_file file==232}

{jd_file file==233}

{jd_file file==234}

{jd_file file==235}

{jd_file file==286}

{jd_file file==289}

{jd_file file==236}

{jd_file file==290}

{jd_file file==238}

{jd_file file==244}

{jd_file file==485}

{jd_file file==247}

{jd_file file==250}

{jd_file file==248}

{jd_file file==251}

{jd_file file==252}

{jd_file file==253}

{jd_file file==292}

{jd_file file==293}

{jd_file file==256}

{jd_file file==294}

{jd_file file==256}

{jd_file file==294}

{jd_file file==295}

{jd_file file==259}

{jd_file file==298}

{jd_file file==260}

{jd_file file==301}

{jd_file file==262}

{jd_file file==263}

{jd_file file==268}

{jd_file file==269}

{jd_file file==302}

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA AS...

Read 34786 times

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: Government City
 • Mtumba Area - Afya Street
 •               P.O.Box 10
 •               40479 Dodoma
 • Tel:        +255 26 216 0270               
 •                +255 737 962 965
 • Email:    info@moe.go.tz
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top