UTANGULIZI
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari. Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekodari ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02) za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari kidato cha I-IV. Aidha kwa waombaji ambao moja ya “Principal Pass”mbili ni somo la Uchumi “Economics”, wanaweza kuomba kozi za fani ambazo ni Michezo (Physical Education and sports), Muziki, Sanaa za Ufundi (Fine Arts), na Sanaa za Maonesho (Theatre and Performing Arts).
AINA YA MAFUNZO NA SIFA
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo
Na |
AINA YA MAFUNZO |
SIFA ZA KUJIUNGA |
CHUO |
MUDA WA MAFUNZO |
1 |
Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati |
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili katika masomo ya Tahasusi za Sayansi, Hisabati na TEHAMA kwa kuzingatia Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kama ifuatavyo: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agricultural Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science. |
Monduli TC, Mandaka TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC, Tabora TC |
Miaka 2 |
2 |
Stashahada ya Sayansi ya Jamii , Biashara na Lugha |
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili kwa kuzingatia masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari Kidato cha I-IV. Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kidato cha I-IV ni : Kiswahili, English, History, Geography, Civics, Commerce na Book keeping. |
Bunda TC, Mtwara (K) TC, Marangu TC, Nachingwea TC, Shinyanga TC, Mandaka TC, Mpuguso TC, Dakawa TC, Butimba TC, Tabora TC, Morogoro TC, Tarime TC, |
Miaka 2
|
3 |
Stashahada ya Ualimu Michezo, Muziki, Sanaa za Ufundi na Sanaa za Maonesho |
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili pamoja na ufaulu wa masomo yaliyoainishwa katika mtihani wa kidato cha IV kwa kila kozi kama ifuatavyo: |
||
(a) Sanaa za Ufundi: masomo ya Fine Arts , Basic Mathematics, Chemistry, History, Physics, English na Civil Engineering. |
Butimba TC |
Miaka 2 |
||
(b) Sanaa za Maonesho: masomo ya English, Literature in English, Kiswahili, Geography na History. |
Butimba TC |
Miaka 2 |
||
(c) Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na masomo ya English, Kiswahili, Physics, Geography, History na Biology. |
Butimba TC |
Miaka 2 |
||
(d) Elimu kwa Michezo: masomo ya Physical Education and sports, Languages, na Biology. |
Butimba TC na Mtwara (K) |
Miaka 2 |
Na. |
AINA YA MAFUNZO |
SIFA ZA KUJIUNGA |
CHUO |
MUDA WA MAFUNZO |
|
1 |
Stashahada ya Elimu Maalum |
Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada au Shahada mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka 2; na awe amefaulu masomo ya Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Sita |
Patandi TC |
Miaka 2 |
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.