TAARIFA KWA UMMA: TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUFUNGULIWA KWA SHULE NA VYUO

Published on Thursday 21 May, 2020 22:56:17

NduguWananchi, kama mnavyofahamu, janaRaiswetuwaJamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, alitoa maelekezo yakuanza kwashughuli mbalimbali ambazo zilisimamishwa iiikuzuia kusambaa   kwaugonjwa wa homa kali ya   mapafu inayosababishwa   na virusi vya corona (COVID-19).   Katika maelekezo   yake Mheshimiwa   Rais, pamoja   na mambo   mengine,   aliagiza   vyuo vifunguliwe na pia wanafunzi wa Kidato cha Sita warejee shuleni kuanzia tarehe 01Juni,2020.

Kufuatia maelekezo hayoyaMheshimiwa Rais,Wizara yaElimu,Sayansi naTeknolojia inapenda kutoautaratibu wautekelezaji kamaifuatavyo:

Wanafunzi waKidato cha Sita

Wizara inazielekeza ShulezotezenyeWanafunzi waKidatochaSitakuanza maandalizi mapema iiiwanafunzi waweze kupokelewa na kuanza masomo rasmi tarehe 01Juni

2020. Hiiina maana kuwa Shule za Bweni ziwe tayari kuwapokea wanafunzi kuanzia siku ya Jumamosi, tarehe 30 Mei, 2020. Shule za kutwa nazo zinaelekezwa  kufanya maandalizi stahiki iiimasomo yaanze rasmi tarehe 01Juni, 2020. Ikumbukwe kwamba ufunguzi   huu wa shule unahusu wanafunzi wa Kidato cha Sita pekee, hautawahusu wanafunzi wa vidato vingine.

Mtihani waKidato chaSita

Wanafunzi wa Kidato cha Sita wataendelea na masomo ambayo yatahitimishwa kwa kufanya Mtihani wao wa mwisho. Mtihani wa Kidato cha Sita utaanza rasmi tarehe 29

Juni, 2020 na kukamilika tarehe16Julai, 2020. Mtihani huo utafanyika sambamba na mitihani ya Ualimu.

Tunatarajia kuwa Baraza la Mitihani laTanzania (NECTA) litatoa matokeo yamitihani hiyo kabla ya tarehe 31Agosti, 2020 ili wanafunzi hao wawe na muda wa kuomba udahili katika Vyuovya Elimu ya Juu. Kwa ratiba hii wanafunzi wataweza kujiungana Vyuo vya Elimu ya Juu katika muda muafaka bila kuathiri ratiba ya masomo kwa mwaka 2020/2021.

Wanafunzi waVvuo vva Kati naVvuoVikuu

Kwa upande wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu, Wizara inaelekeza navyo vianze maandalizi ili viweze kupokea wanafunzi kuanzia tarehe 01Juni 2020. Nazielekeza mamlaka za vyuo hivyo, kwa maana ya Mabaraza na Seneti kupanga ratiba za masomo kwa lengo la kufidia muda ambao wanafunzi walikuwa nyumbani na vyuo vyote vitapaswa kuwasilisha ratiba zao kwa mamlaka husika yaani Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili mwaka huu wa masomo ukamilike kwa wakati muafaka bila kuathiri ratiba za masomo ya mwaka 2020/2021.

Mikopo yaWanafunzi waElimuvaJuu

Wizara inapenda kuwahakikishia wanafunzi naVyuo vya Elimu ya Juu kuwa Serikali ilishatoa jumla ya Shilingi Bilioni   122.8 ambapo Shilingi Bilioni   63.7 ni kwaajili ya chakula na malazi; na Shilingi Bilioni   59.1 ni ada za wanafunzi. Hivyo nazielekeza mamlaka za Vyuo Vikuu kuhakikisha kuwa nyaraka zote muhimu zinazohitajika ili kupokea fedha toka Bodi ya Mikopo zinaandaliwa na kuwasilishwa kabla ya tarehe28/5/2020.   Hii itawezesha Bodi ya Mikopo kutuma fedha kwa wakati muafaka kabla wanafunzi hawajafika vyuoni. Aidha naelekeza piaVyuo Vikuu viweke maofisa wa kutosha kwenye eneo la ugawaji wa mikopo kwa wanafunzi ili wanufaika wapate fedha zao mapema na kuwawezesha kusoma kwa utulivu ikizingatiwa watapaswa kuwa madarasani kwa muda mrefu zaidi ilikufidia siku.

Kwa upande mwingine Serikali inaviagiza Vyuo Vikuu vyote kuwasilisha Bodi yaMikopo nyaraka zao za maombi ya malipo ya ada za wanafunzi (yaani tuition fees) ilimalipo hayo yafanyike mapema ilishughuli zautawala katika vyuo ziweze kuendelea bila pingamizi lolote.

Tahadhari kuhusu Virusi vya Corona

Wizara inapenda kuelekeza shule zote zenye Wanafunzi wa Kidato cha Sita naVyuo vyote  vitakavyofunguliwa  kuanzia tarehe 01/0612020 kuhakikisha wanazingatia maelekezo vote kuhusu kujikinga na Virusi vya Corona.   Shule pamoja na Vyuo vinapaswa kuandaa vifaa vya kunawia mikono kwenye maeneo muhimu kama vile madarasa, kumbi za mikutano na mabwalo ya chakula.

Hitimisho

Wizara inapenda kutoa wito kwa walimu parnoja na wanafunzi kuhakikisha wanajituma katika masomo yao iiiwaweze kukamilisha mihtasari kwa wakati bila kuathiri mwaka wa masomo2020/2021.

Read 12817 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 216 0270               
  •                +255 737 962 965
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top