Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ipo katika maandalizi ya kutekeleza Mradi wa Kuinua Ubora wa Elimu ya Awali na Msingi - BOOST kwa lengo la kuboresha usawa wa elimu katika ujifunzaji kwa ngazi ya elimu awali na msingi nchini.
Utekelezaji wa mradi utazingatia miongozo ya usalama wa mazingira na jamii ambayo ni: Environmental and Social Commitment Plan – ESCP; Labour Management Procedures – LMP; na Stakeholder Engagement Plan – SEP ambayo inapatikana kupitia tovuti ya WyEST www.moe.go.tz.
{jd_file file==490}
{jd_file file==491}
{jd_file file==492}
Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Dunua imeandaa kikao cha wadau kwa ajili ya kupokea maoni ya wadau yatakayowezesha uboreshaji wa rasimu ya miongozo hiyo. Kikao hicho kitafanyika tarehe 15 Oktoba, 2021 kwa njia ya mtandao kupitia kuanzia Saa 9:00 asubuhi. Aidha, wadau wanaweza kushiriki kikao hiki katika ukumbi wa St. Gaspar- Mkoani Dodoma.
Wadau |
Tarehe |
Taasisi na Wakala wa Serikali, Jumuiya za wataaluma vyuoni, Asasi zisizo za Serikali, Mashirika, Makampuni, watu binafsi na wadau wa maendeleo |
15 Oktoba, 2021 |
Kwa kuzingatia umuhimu wa miongozo hiyo, WyEST inawaalika wadau kushiriki kikao hiki kwa ajili maoni kabla miongozo hiyo haijapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Baruapepe kwa anuani ifuatayo: -