PROF. MKENDA AKUTANA NA KAMATI ZA MABORESHO YA SERA NA MITAALA

Published on Wednesday 16 November, 2022 10:15:36

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Novemba 15, 2022 amekutana na Menejimenti ya Wizara hiyo pamoja na Kamati za Kitaifa za Maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo na Mitaala Jijini Dodoma.

Lengo la Kikao hicho ni kupokea taarifa ya maendeleo ya kazi za  Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 pamoja na ile ya Marekebisho ya Mitaala ya Elimu msingi na Ualimu.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba pamoja na Wajumbe wa Kamati za Sera na Mitaala.

Read 629 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 216 0270               
  •                +255 737 962 965
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top