MKUTANO WA KIMATAIFA WA ELIMU JIJINI LONDON-UINGEREZA

Published on Monday 20 January, 2020 22:25:24

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na baadhi ya wataalamu wa elimu kutoka Tanzania wakiwemo kutoka Washirika wa Maendeleo kutoka "DFID" Tanazania na British Coucil Tanzania wanashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Elimu jijini London Uingereza ambapo ajenda kuu ya mkutano ni nini kifanyike kuboresha Elimu ndani ya kikazi kimoja "One Generation"

Mkutano huo unawaleta pamoja Mawaziri wenye dhamana ya Elimu na wataalam katika Sekta elimu kutoka nchi 120 ambapo pia watajadili kuhusu mfumo sahihi wa upimaji uelewa wa wanafunzi na kama matokeo ya Mwanafunzi yanatokana na Mwanafunzi mwenyewe, Mfumo, Walimu au Mitaala.

Mengine yatakayojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na uboreshaji Mazingira ya utoaji elimu kwa ajili ujifunzaji, uboreshaji Elimu jumuishi, uimarishaji Elimu ya Ufundi katika kuongeza Vijana wenye ujuzi, umuhimu wa vipaumbele vya elimu katika ngazi zote za elimu kuwiana, maendeleo ya Teknolojia yanavyochagiza na kutumika katika ujifunzaji na ufundishaji, umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za Kitaifa za Sekta na pia umuhimu wa uwekezaji katika elimu ya awali katika ujifunzaji.

Read 2855 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022