Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili Ndani na Nje ya Nchi 2022 - 2030

Published on Tuesday 22 November, 2022 16:09:45

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo tarehe 20 Novemba 2022, imeshiriki na Kutoa Mada katika Mkutano wa Mheshimiwa Rais Wizara na Mabalozi Tarehe 14 Hadi 21 Novemba, 2022 wenye Kauli mbiu "Muelekeo Mpya Karika Kuimarisha Diplomasia ya Uchumi". Mkutano huu pamoja na mambo mengine wamejadili Mada "Nafasi ya Balozi Katika Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili Ndani na  Nje yabNchi 2022 - 2030". 
Ambayo ilikusanyisha Jopo la Washiriki wanne(4) Bi. Hilda Bukozo,ndc kutoka WyEST alietoa Mada ya MPANGO MKAKATI WA WyEST KATIKA KUBIDHAISHA LUGHA YA KISWAHILI NJE YA NCHI KWA NJIA YA MAFUNZO. Pia Bi Consolata Mushi (BAKITA) na  Dr Mwanahija Ali Juma (BAKIZA) Waliwasilisha "Mpango Mkakati wa kubidhaisha Kiswahili nje ya nchi 2022 -2032". Jopo hilo liliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Sayd Othman Yakub (mtoa mada mkuu) alie fungua mada kwa lisara fupi na kugawa vitabu vya kiswahili kwa Mabalozi mwishoni mwa mawasilisho hayo. Mkutano huu uliendeshwa na Mh. Balozi Mstaafu Rajabu Gahama.

Uwasilishi huu wa WyEST umekuja kama sehemu ya Jitihada za Wizara kuendana na kasi ya soko la Kiswahili nje ya mipaka, baada ya uhitaji wa mikataba ya kiswahili kwa njia ya mafunzo kuongezeka. Hii pia ni kutii wito wa Mh. Rais kwa Wizara,Taasisi na Wadau kuwekeza kwenye kufundisha na kujifunza lugha ya kiswahili ndani na Nje ya Nchi.

Idara  za WyEST na Taasisi zake zimepewa jukumu la kusimamia harakati hizi kwakukutanisha wataalam Kitaifa na wadau wa Kiswahili ili kukamilisha malengo yaliyokusudiwa ya Diplomasia ya Uchumi kwa njia ya mafunzo ya kiswahili.

Bi. Hilda Bukozo ametoa wito kwa niaba ya  Katibu Mkuu  WyEST na kywashirikisha Mabalozi, Diaspora na jukwaa za kidiplomasia kufanya tafiti za Kimkakati kung'amua uhitaji uliopo nchi za uwasilishi wao na kushauri jinsi gani lugha ya kiswahili inavyoweza kuwafikia kwa njia ya mafunzo, na kubaini hatua endelevu za mikakati hiyo(sustainable plans)

Amidi wa Mabalozi Mh. Asha Rose Migoro, pamoja na mwenyekiti wa mkutano Katibu Mkuu Nje Joseph Sokoine wamesifia jitihada hizi na kuipongeza Wizara kwa maandalizi na uwasilishi.

Read 541 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 216 0270               
  •                +255 737 962 965
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top