MAKABIDHIANO YA OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Published on Monday 13 March, 2023 11:37:08

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Wizara itaendeleza misingi iliyoachwa na viongozi waliotangulia katika Wizara hiyo ili kuwezesha kutimiza malengo yake.
 
Prof. Nombo amesema hayo Machi 13, 2023 jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Francis Michael ambapo amesema nyaraka alizokabidhiwa kwake ni nyenzo muhimu kwa ajili ya uendelezaji wa kazi za Wizara.
 
Katibu Mkuu huyo amemshukuru Dkt. Michael kwa kumlea wakati akiwa Naibu Katibu Mkuu  kwani kupitia yeye amejifunza mengi. Aidha amemuomba kuwa balozi wa sekta ya Elimu Sayansi na Teknolojia katika Mkoa wa Songwe ambako kwasasa ni  Mkuu wa Mkoa huo.
 
Naye Dkt Francis Michael amempongeza Katibu Mkuu Nombo kwa kuaminiwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba yupo tayari kutoa ushirikiano  na ushauri wowote atakapoitajika kufanya hivyo.

Read 294 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 216 0270               
  •                +255 737 962 965
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Kituo cha Huduma kwa Mteja