KUTOA MAONI YA KUBORESHA MTAALA WA ELIMU MSINGI NI HAKI YA KILA MTANZANIA

Published on Sunday 11 July, 2021 00:44:09

Imeelezwa kuwa mikutano ya wadau ya kukusanya maoni juu ya uboreshaji wa mitaala ya elimumsingi ni muhimu kwa Taifa kwa kuwa itawezesha wadau kutoa maoni ya uboreshaji wa mitaala hiyo ili itoe ujuzi na maarifa yatakayoweka msingi madhubuti wa elimu nchini.?
?
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako mwishoni mwa wiki Zanzibar wakati akifungua mkutano wa wadau kuhusu maoni ya kuboresha mitaala ya elimu ya sekondari kidato cha i-vi ili kukidhi mahitaji ya Tanzania ya uchumi wa kati na viwanda, ambapo amesema mitaala bora itasaidia kujenga msingi imara wa elimu kwa kuwawezesha wahitimu kuwa na ujuzi na maarifa stahiki na kuwajengea ari ya kupenda kujifunza zaidi ili kuweza kumudu kikamilifu mazingira wanayoishi na shughuli za maendeleo wanazozifanya.?
?
“Mitaala bora ya ngazi hii itasaidia kujenga msingi imara wa elimu kwa ngazi zinazofuata. Msingi huo utawawezesha wahitimu kuwa na ujuzi na maarifa stahiki na kuwajengea ari ya kupenda kujifunza zaidi ili kuweza kumudu kikamilifu mazingira wanayoishi na shughuli za maendeleo wanazozifanya”. Amesisitiza Waziri Ndalichako?
?
Waziri huyo amewasihi Wazanzibari kutoa maoni kikamilifu katika uboreshaji wa mitaala ya elimu ya sekondari kwa kupendekeza maeneo wanayoyaona yanayopaswa kufanyiwa maboresho ili kuwa na elimu iliyojikita kwenye ujuzi. Amesema katika karne ya 21, dunia imeshuhudia mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia yaliyoleta utandawazi ambao moja ya athari zake ni kuongezeka kwa ushindani katika soko la ajira na kuwa na wahitimu wabunifu wanaoweza kutumia sayansi na teknolojia kubuni vyanzo zaidi vya kukuza na kuimarisha uchumi wetu.?
?
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Saidi amesema maoni yaliyotolewa na wadau katika mkutano huo ni muhimu na wao kama viongozi wameyapokea na kwamba yatafanyiwa kazi na wataalam na kisha kurudisha mrejesho kwa wadau hao kuhusu nini kinaendelea katika maboresho ya mitaala ya elimumsingi.?
?
Naye Mdau Henry Kulaya amesema mitaala iliyopo haina mapungufu makubwa kama ilivyokuwa ikifikiriwa, ameshauri kuongeza umahiri wa watoa elimu kwa kutoa mafunzo kazini kwa walimu ili waweze kutekeleza vyema mitaala. Pia amesisitiza kuwepo kwa elimu ya ufundi na ujuzi katika ngazi zote za elimu ili kuwawezesha watoto kuwa na uwezo wa kujitegemea kutokana na ngazi aliyopo.?
?
Naye mdau wa elimu Amina Duliwaza amesema katika? utekelezaji wa mitaala hakuna sehemu ambayo inaongelea ufundishaji wa lunga ya alama jambo ambalo limeleta changamoto kwa watoto wenye matatizo ya kusikia kwani hata walimu waliopo shuleni hawaijui lugha hiyo na wala hawaitumii. Hivyo ameshauri kuona namna ya kuwekwa vipengele vya ufundishaji wa lugha ya alama katika mitaala.?

Read 1402 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022