Kutokana na mwitikio Mkubwa wa wadau toka ndani na nje ya Nchi wa kushiriki Kongamano la Elimu, Wizara imesogeza mbele tarehe ya kufanyika kongamano hilo ili kutoa nafasi kwa wadau zaidi kushiriki na kuendelea kutoa maoni .
Tarehe mpya ya kongamano itatangazwa hivi karibuni. Tunaendelea kukaribisha maoni na kusajili kushikiri kongamano hili lenye lengo ya kujadili maboresho ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 na mabadiliko ya Mitaala yetu.
Wizara inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza nia ni kupanua zaidi wigo wa ushiriki na upokeaji maoni.
Endelea kutuma moni kupitia maoniyawadau@tie.go.tz au info@moe.go.tz au tupigie kwa Namba 0735041169 tutakusikiliza.
#TunaboreshaElimuYetu