Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yapokea taarifa ya maendeleo ya kazi ya uboreshaji Mitaala katika ngazi zote za elimu nchini

Published on Monday 08 November, 2021 18:31:49

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloja leo Novemba 8, 2021 jijini Dodoma imefanya kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kutoa taarifa ya maendeleo ya kazi ya uboreshaji Mitaala katika ngazi zote za elimu nchini.

Uwasilishwaji wa taarifa hizo umefanywa na Wakuu wa Taasisi zinazohusika na mitaala nchini ambao ni Dkt. Aneth Komba kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ambaye aliwasilisha kwa upande wa Mitaala ya Elimumsingi, Mtendaji Mkuu Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Adolf Rutayuga ambaye aliwasilisha uboreshaji wa Mitaala ya elimu ya ufundi na Vyuo vya Kati na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)Tanzania Profesa Charles Kihampa aliewasilisha kuhusu Mitaala ya Elimu ya Juu.
 
Baada ya mawasilisho hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Stanlaus Nyongo amesema lengo la Kikao hicho ilikuwa ni kupata taarifa ya maendeleo ya zoezi la uboreshaji wa mitaala hiyo ili Kamati yake iweze kurejesha taarifa hiyo kwa wabunge wengine.

Mwenyekiti huyo amesema pamoja na kwamba mchakato bado unaendelea wa kuboresha mitaala ya elimu, kazi hiyo imefanyika na inaonekana ingawa bado haijafika mwisho. Hivyo ameitaka Wizara kuwasilisha taarifa hizo kwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2021 ili nao waweze kutoa maoni.

Read 261 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top