WAZIRI NA KATIBU MKUU WAPOKELEWA NA WATUMISHI WA WIZARA

Published on Tuesday 11 January, 2022 12:02:32

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Eliamani Sedoyeka leo Januari 10, 2022 wameripoti katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ikulu ya Chamwino.

Viongozi hao wamepokelewa na watumishi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Omari Kipanga na Manaibu Katibu Wakuu, Profesa James Mdoe na Profesa Carolyne Nombo.

 Akizungumza na watumishi hao Waziri Mkenda amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuwa wabunifu katika kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya Elimu.

Naye Katibu Mkuu Profesa Sedoyeka amesema kipaumbele chake ni matumizi ya teknolojia katika Elimu ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na kuwataka watumishi hao kushirikiana nae katika kuhakikisha sekta ya elimu, sayansi na teknolojia inaleta matokeo chanya katika uchumi wa nchi.

Read 634 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top