WAZIRI MKENDA ATOA FURSA KWA WAANDISHI WA VITABU NCHINI

Published on Thursday 21 April, 2022 13:25:43

KWA  WAANDISHI WA VITABU  NCHINI
 
Na WyEST
DODOMA
 
# Bajeti kutengwa kusadia uchapishaji wa miswada mahiri
 
#Miswada kushindanishwa
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema Wizara itatenga bajeti kwa ajili ya mtu yeyote mwenye muswada wa kuandika riwaya ambazo zitashindanishwa na muswada ambao utashinda utagharamiwa uchapishaji wake na Wizara. 
 
Amesema hayo Jijini Dodoma alipokutana na wawakilishi wa Mwandishi wa Kitabu cha Hesabu kilichoandikwa kwa kutumia mitaala ya Kenya, Uganda na Tanzania, David Inzofu ambapo amesema lengo ni kuona kunakuwa na Watanzania wengi wanaojitokeza kuandika vitabu. 
 
Waziri Mkenda amemuagiza Kamishna wa Elimu kuhakikisha kitabu hicho kinapitiwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ili kama kuna sehemu ya kuboresha iweze kuboreshwa kwa lengo la kumsaidia mwandishi huyo ili kuongeza hamasa kwa Watanzania wengi zaidi kuandika vitabu na kuhamasisha usomaji.
 
“Tunataka kusaidia waandishi ambao wanataka kuandika riwaya. Tunaposema elimu yetu tunataka iakisi mahitaji ya nchi yetu na utamaduni wetu tungependa pamoja na wanafunzi kusoma vitabu vya nje wasome pia vilivyoandikwa na Watanzania,” amesema Prof. Mkenda.
 
Amesema kumekuwepo na maoni ya kutumia Kiswahili kufundishia katika siku zijazo, hivyo kunahitaji maandalizi ili kuweza kufika huko, Watanzania wenyewe waandike vitabu wawe tayari, uwezo na uzoefu wa kutafsiri vitabu vya Kiingereza kuwa vya Kiswahili.
 
“Tungependa kukuza Kiswahili na hii inahitaji maandalizi, hivyo lazima kuwe na vitabu vingi vya Kiswahili, huwezi kuanza kutumia lugha ya Kiswahili huku vitabu vikiwa vya Kiingereza.  Huyu mwalimu David Inzofu nafurahi kwamba ametafsiri hiki kitabu kwa Kiswahili itabidi tumsaidie ili Baraza la Kiswahili lihakiki kitabu hicho,” ameongeza Waziri Mkenda.
Read 590 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022