Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema jukumu la wizara ni kuhakikisha inaboresha taaluma na mafunzo yanayotolewa ili yawe na tija katika kuandaa vijana wanaoweza kuajiriwa na kujiajiri kulingana na mahitaji ya Taifa.
Naibu Waziri ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa akifunga Mkutano wa .... wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo ambapo amesema wizara inapaswa kukidhi kiu ya watanzania ya kutaka kuona vijana wanapata taaluma zenye tija.
“Hata kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii hoja hii iliibuka katika maeneo mengi ya kutaka vijana waandaliwe kwa kupatiwa mafunzo yenye kuwawezesha kujitegemea kwa kufanya kazi” amesema Naibu Waziri.
Aidha, Mhe. Kipanga amevitaka vyama vya TUGHE na CWT kuendelea kushirikiana na uongozi wa wizara katika kuhakikisha watumishi wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi pamoja na kulinda nidhamu na umoja wa wizara.