Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof Carolyne Nombo leo Machi 23, 2023 wamekutana na Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu kwa lengo la kujadili maandalizi ya utoaji wa tuzo hizo
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma Prof Mkenda ameipongeza kamati hiyo kwa kazi kubwa waliofanya.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Salma Omar Hamad ameeleza kuwa maandalizi ya utoaji tuzo hizo yanaendelea na kwamba hafla ya utoaji tuzo hizo itakuwa Aprili 13, 2023
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanzisha mashindano ya Uandishi Bunifu ili kutambua na kutoa chachu kwa watanzania kuandika .
Mashindano hayo kwa mwaka 2023 yalizinduliwa Septemba 12, 2022 .