SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO WAOMBAJI WA SKOLASHIPU ZA JUMUIYA YA MADOLA NCHINI UINGEREZA (COMMONWEALTH SCHOLARSHIP 2020) ITAKAYOFANYIKA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO, MOROGORO TAREHE 20 OKTOBA 2019
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na British Council imeandaa Semina elekezi ya kuwajengea uwezo waombaji wa Skolashipu za Jumuiya ya Madola kwa mwaka 2020, kwa waombaji walioko mkoani Morogoro na maeneo ya jirani, itakayofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) siku ya Jumapili, tarehe 20 Oktoba 2019 katika Ukumbi wa New Lecture Theatre 9 (NLT9) kuanzia saa saba mchana (07.00) hadi saa kumi jioni (10.00).
Lengo la Semina hii pamoja na mambo mengine ni kuwaongezea uwezo na weledi waombaji wa skolashipu hiyo kwa hatua za shahada za Uzamili na Uzamivu.
Kwa tangazo hili, yeyote mwenye nia na ufadhili huo anakaribishwa kuhudhuria.
Nyote mnakaribishwa.