SERIKALI YATEKELEZA KWA VITENDO UBORESHAJI ELIMU YA UALIMU- CHUO CHA UALIMU KABANGA CHAJENGWA UPYA

Published on Monday 19 July, 2021 08:43:05

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango amesema ujenzi wa majengo mapya ya Chuo cha  Ualimu Kabanga ni moja ya mikakati ya Serikali kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu ya Nchini.
 
Ameyasema hayo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati wa kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa  majengo mapya ya Chuo hicho ambapo amewataka walimu tarajali kusoma kwa bidii kwa kuwa sasa miundombinu imeboreshwa.

Kiongozi huyo amesema ameridhishwa na taarifa Ujenzi huo kwa  kuwa umezingatia matumizi Bora ya Nishati mbadala na nafuu na pia uhifadhi wa mazingira.  Aidha amesema ni vizuri chuo hicho kikachukua tahadhari zote za kuzuia majanga yakiwemo ya moto na kuwataka  walimu tarajali wa Chuo cha Ualimu Kabanga watakaohamia katika majengo mapya ya Chuo hicho  kutunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu. 

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Mradi  huo mpaka utakapokamilika utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 11 na kwamba umefadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia Programu ya Kuimarisha Elimu ya Ualimu (TESP) na kwamba ujenzi utakapokamilika utaongeza udahili kutoka 400 hadi 800.

Nae Balozi wa Canada Pamela O'dennel amesema ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga ni wa kisasa unaozingatia mbinu za kimazingira na hivyo kuwa na  nafasi kubwa ya kuchangia juhudi za Serikali za kukabiliana changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi. Pia itachangia jitihada za maendeleo endelevu ambayo ni nishati safi usawa wa kijinsi na kupambana na madiliko ya tabia nchi na kufanya chuo hicho kuwa cha karne.

Read 1355 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top