SERIKALI YAENDELEA KUSAMBAZA VITABU VYA KIADA MASHULENI

Published on Friday 28 February, 2020 14:48:24

Serikali imezitaka shule za umma na zisizokuwa za serikali kutumia vitabu vya kiada na ziada vyenye ithibati katika kufundishia na kujifunzia ili kuhakikisha maudhui ya elimu wanayopatawanafunzi yanakuwa bora na kukidhi vigezo.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kazi ya kusambaza vitabu vya kiada kwa shule za msingi zinazotumia lugha ya kiingereza katika kufundishia na vitabu vya nukta nundu kwa darasa la I-V na Kidato cha nne.

"Vitabu hivi ndio moyo wa Elimu hivyo walimu na wanafunzi wanapaswa kuvitumia wakati wa kufundisha na pia wanafunzi wavitumie kwa kujifunza na sio kuviweka stoo" amesisitiza Ole Nasha.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt Aneth Komba ametoa rai kwa waandishi binafsi wa vitabu kupeleka vitabu katika ofisi za TET kwa ajili ya kupitiwa na kupewa ithibati.

Alimesisitiza kuwa TET inatambua mchango mkubwa wa wachapaji binafsi ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa vitabu vya ziada kwa wanafunzi.

Jumla ya nakala 1,305,950 zilizochapwa zitazambazwa katika shule za serikali zinazotumia lugha ya kiingereza katika kujifunzia na kufundishia kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu.

Read 2002 times

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Government City
  • Mtumba Area - Afya Street
  •               P.O.Box 10
  •               40479 Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    info@moe.go.tz
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
Tanzania Census 2022