Maafisa Habari wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Taasisi zake wameshiriki kikao cha 18 cha maafisa habari na mawasiliano wa Serikali chenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuwasiliana kimkakati na kuwa injini ya maendeleo.
Kikao kazi hicho kimefunguliwa leo Machi 27, 2023 jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni "Mawasiliano ya Kimkakati injini ya Maendeleo."