JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 2121600
Fax: 022-2113271 Elimu Tz
KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI YA MAFUNZO YA MUDA MFUPI YA UALIMU KWA WATAKAOKWENDA KUFUNDISHA SHULE ZA SEKONDARI
MACHI HADI APRILI 2007
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi 6,000 za mafunzo maalumu ya ualimu ya muda mfupi (Wiki Nne) kwa wahitimu wa kidato cha SITA wenye ufaulu wa kiwango cha “principal pass” mbili kwenye masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari. Maombi yanawahusu pia waombaji waliosomea kozi za ufundi (Full Technician Course-FTC) na Elimu ya Biashara (Business Education). Aidha, mwombaji awe ameshinda kidato cha sita, aoneshe jinsi (Ke/Me) pamoja na umri wake. Mafunzo yataendeshwa kuanzia tarehe 12/03/2007 hadi 07/04/2007. Maombi ya kujiunga na mafunzo yatumwe katika vyuo vya ualimu kwa kuzingatia mkoa anakotoka mwombaji kama ifuatavyo:
Chuo |
Mikoa |
Idadi ya nafasi |
Chuo cha Ualimu Morogoro, |
Dar es Salaam |
850 |
Chuo cha Ualimu Mpwapwa, |
Singida |
800 |
Chuo cha Ualimu Tabora, |
Tabora |
400 |
Chuo cha Ualimu Tukuyu, |
Mbeya |
550 |
Chuo cha Ualimu Butimba, |
Mwanza |
850 |
Chuo cha Ualimu Kleruu, |
Iringa |
300 |
Chuo cha Ualimu Monduli, |
Arusha |
550 |
Chuo cha Ualimu Bunda, |
Kagera |
450 |
Chuo cha Ualimu Korogwe,. |
Tanga |
850 |
Chuo cha Ualimu Mtwara(K), |
Ruvuma |
400 |
A: MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI
B: GHARAMA ZA MAFUNZO:
Watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo watajigharimia nauli kwenda chuoni na watarejeshewa nauli hiyo pamoja na nauli ya kwenda kwenye wilaya watakazopangiwa kufundisha. Serikali itagharimia ada ya mafunzo, vifaa vya mafunzo na chakula kwa muda wote wa mafunzo. Aidha, Mwanafunzi atajigharimia vifaa vya usafi na malazi (shuka, mto), vyombo vya kulia chakula na fedha za matumizi binafsi.
C: AJIRA BAADA YA MAFUNZO
Wahitimu wa Mafunzo haya maalumu ya Ualimu watapatiwa leseni ya kufundisha kwa miaka minne (4) na wtaajiriwa katika shule za sekondari za Serikali.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28/02/2007. Unaweza pia kusoma tangazo hili katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz
Hamisi O. Dihenga
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P.9121, DAR ES SALAAM