JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 2121600
Fax: 022-2113271 Elimu Tz
NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA: JULAI 2007/2008
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anatangaza nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kama ifuatavyo:
A: MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI
B: KUAJIRIWA BAADA YA MAFUNZO
C: GHARAMA ZA MAFUNZO: Ada kwa Mafunzo ya Ualimu (tarajali) ngazi ya Cheti (IIIA) na Stashahada kwa kila mwaka wa masomo ni shs. 150,000/=.
D: Aina ya mafunzo yatakayotolewa na sifa zinazotakiwa ni kama ifuatavyo:
NA |
MAFUNZO |
SIFA ZA WAOMBAJI |
1. |
STASHAHADA YA UALIMU (TARAJALI): MUDA WA MIAKA 2 |
Awe amefaulu kidato cha VI kwa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘subsidiary’ moja katika masomo yanayofundishwa shule za sekondari. AU awe na cheti cha FTC katika masomo ya Sayansi na Hisabati. |
2. |
STASHAHADA YA UALIMU (KAZINI): MUDA WA MIAKA 2 |
|
3. |
STASHAHADA YA UALIMU (ELIMU MAALUM): MUDA WA MIAKA 2 |
(a) Awe mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu(IIIA) cha Elimu Maalum, na ambaye amefaulu masomo mawili Kidato cha Sita. AU |
4. |
STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MIAKA 2 |
(a) Awe mwalimu mwenye Cheti cha: Ualimu Daraja IIIA, Sayansi Kimu na awe ameshinda kwa kiwango kisichopungua “Principal Pass” moja na “Subsidiary” katika masomo ya: Baiyolojia, Kemia na Sayansi Kimu katika mitihani ya Kidato cha VI. AU |
5. |
MAFUNZO YA STASHAHADA YA UALIMU (MICHEZO, MUZIKI, SANAA MAONESHO/UFUNDI). MUDA WA KOZI: MIAKA 2. |
AU
(c) Waombaji wote watakaochaguliwa watafanyiwa usaili kabla ya kujiunga na mafunzo. |
6. |
MAFUNZO YA CHETI CHA UALIMU (SAYANSI KIMU): MUDA WA MWAKA 1 |
(a) Awe mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja IIIA. |
7. |
MAFUNZO YA CHETI CHA UALIMU (ELIMU MAALUM): MUDA WA MWAKA 1 |
(a) Awe mwalimu mwenye cheti cha ualimu daraja la IIIA. |
8. |
DIPLOMA (Technical Education.) |
Awe amefaulu na kupata cheti cha FTC kutoka vyuo vya Ufundi Arusha, Mbeya, Dar es Salaam au sifa inayolingana. |
9. |
DIPLOMA (Agriculture Education) |
Awe amefaulu kidato cha VI kiwango cha angalau “Principal Pass” moja na “Subsidiary” katika masomo ya Baiyologia na Kilimo au sifa inayolingana. |
10. |
DIPLOMA (Commerce/Accauntancy) |
Awe amefaulu kidato cha VI, kiwango kisichopungua “Principal Pass” moja na “Siubsidiary’” katika masomo ya Biashara na Uhasibu (Accountacy) |
11. |
CHETI NA MAFUNZO MAALUM YA MUDA MFUPI (LESENI YA KUFUNDISHA SHULE ZA SEKONDARI) |
Awe amefaulu kidato cha VI kwa kiwango kisichopungua “Principal Pass” moja na ‘Subsidiary’ moja. Kipaumbele ni kwa masomo ya Hisabati, Sayansi na Kiingereza. |
E. Angalizo; Waombaji wenye ufaulu chini ya Principal Pass mbili watapaswa kurudia mitihani ya Kidato cha Sita wakiwa mwaka wa kwanza chuoni ili waweze kuendelea na mwaka wa pili. Aidha, waombaji wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha watapewa kipaumbele.
F: Maombi yote yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu).
MAJIBU YATATOLEWA KWA WATAKAOTEULIWA TU.
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 25/05/2007.