Majukumu Makuu ya Wizara

 • Majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni:-

  • kutunga na Kutekeleza Sera za Elimu, Sayansi, Utafiti, Huduma za Maktaba, Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Uendelezaji wa Mafunzo ya Ufundi;
  • kuendeleza Elimumsingi kwa Kutoa Ithibati ya Mafunzo ya Ualimu na Maendeleo ya Kitaalamu ya Walimu;
  • kubainisha Vipaji na Kuviendeleza;
  • kusimamia Uendelezaji wa Mafunzo katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi;
  • kusimamia Mfumo wa Tuzo wa Taifa;
  • kuainisha Mahitaji ya Nchi katika Ujuzi na Kuuendeleza;
  • kuweka Viwango vya Taaluma ya Ualimu;
  • kusimamia Ithibati na Uthibiti wa Shule;
  • kusimamia Huduma za Machapisho ya Kielimu;
  • kutegemeza/Kuimarisha Utumiaji wa Sayansi, Uhandisi, Teknolojia na Hisabati;
  • kuendeleza Wataalamu wa ndani katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu;
  • utafiti katika Sayansi na Teknolojia;
  • uendelezaji wa Rasilimaliwatu na Uongezaji Tija ya Watumishi walio chini ya Wizara; na
  • kuratibu Shughuli za Idara, Mashirika, Wakala, Programu na Miradi iliyo chini ya Wizara.

Read 33568 times

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…