• KUFANYA MALIPO KUPITIA MFUMO WA SERIKALI WA GePG

    

  Wizara, imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato ya Serikali kwenye makusanyo yake yote ya mapato kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Kanda za Uthibiti Ubora wa Shule. Hivyo mteja atapaswa kufika au kuwasiliana na kituo husika anachotaka kufanya malipo ili kupata namba ya utambulisho wa malipo husika (Payment Control Number) kabla ya kufanya malipo

  1. Malipo yanaweza kufanywa kwa njia ya kibenki kwa kufuata hatua zifuatazo;

  1. Unapopata kumbukumbu ya malipo (Control Number);
  2. Tembelea Tawi lolote la Benki ya CRDBNMB na NBC;
  3. Baada ya kuwasili kwenye benki, mpe mtoa huduma wa dirishani namba kumbukumbu ili kukamilisha mchakato wa malipo yako.

   

  2. Malipo yanaweza pia kufanywa kwa njia ya mtandao wa simu za mikononi (M-pesa, Tigo Pesa na Airtel Money) kwa kufuata hatua zifuatazo;

  1. Kupitia simu yako, piga *150*00#, au *150*01# au *150*60#;

  (Kupitia M- pesa, Tigo Pesa na Airtel Money);

  1. Chagua ‘Lipia malipo (Pay-Bills)’;
  2. Chagua ‘Malipo ya Serikali’;
  3. Chagua ‘Ingiza namba ya malipo’ na uingize namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number);
  4. Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa;
  5. Thibitisha muamala wako kwa kuingiza neno au namba yako ya siri; na
  6. Hifadhi ujumbe wa simu uliopokea kama ushahidi wa malipo endapo utahitajika kuonyesha kwa kituo husika.

   
 • Sayansi Teknolojia na Ubunifu

  Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi na ina sehemu mbili (2) zifuatazo: -

  1. Sehemu ya Utafiti na Maendeleo; na
  2. Sehemu ya Sayansi na Teknolojia.

  Lengo

  Kutoa sera na miongozo juu ya utafiti na maendeleo, na ubunifu likiwa na lengo la kuibadilisha nchi kuwa yenye jamii iliyoelimika.

  Majukumu

  1. Kuandaa, kurekebisha na kufuatilia utekelezaji wa sera, miongozo na viwango husika vya sayansi, teknolojia, na ubunifu;
  2. Kuhamasisha ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia nchini;
  3. Kuweka mazingira mazuri ya kiutafiti kuhusu sayansi, teknolojia na ubunifu nchini;
  4. Kuwaandaa wafanyakazi wenye uweledi juu ya sayansi na teknolojia kulingana na wizara / sekta husika;
  5. Kuanzisha na kusimamia taasisi za sayansi na teknolojia nchini;
  6. Kuunda na kuratibu utekelezaji wa mfumo wa ubunifu wa kitaifa;
  7. Kuhamasisha tasnia na sekta binafsi ili kuongeza uwekezaji wake katika maendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu;
  8. Kuanzisha na kusimamia utendaji wa mfuko wa Taifa wa Utafiti.

   

 • Sehemu ya Utafiti na Maendeleo

   

  Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi, na inafanya shughuli zifuatazo: -

  1. Kuandaa na kuhakiki sera ya taifa ya utafiti na kufuatilia utekelezaji wake;
  2. Kuhamasisha maendeleo ya ujuzi wa utafiti na rasilimali watu katika utafiti;
  3. Kuhamasisha matumizi sahihi ya rasilimali za utafiti kupitia mipango ya kitaasisi ya kimkakati, ushirikiano kati ya taasisi na sekta husika;
  4. Kuwezesha shughuli za utafiti wa kiushindani zinazohusiana na tasnia na sekta binafsi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi;
  5. Kuanzisha na kuratibu maendeleo ya Masuala ya Utafiti ya Taifa (NRA);
  6. Kuendeleza na kuratibu mkakati wa utafiti na maendeleo, halikadhalika usambazaji wa matokeo ya utafiti na matumizi yake;
  7. Kuwezesha uanzishwaji na kusimamia uongozi wa mfuko wa utafiti wa kitaifa;
  8. Kujenga mazingira na mfumo bora wa ushiriki wa sekta binafsi katika utafiti;
  9. Kuendeleza utaratibu wa kukuza ushirikiano katika utafiti kati ya taasisi mbalimbali;
  10. Kuhamasisha ushirikiano kati ya sekta na biashara ili kutambua mahitaji na rasilimali za sekta hizi na kufafanua mipango ya utafiti husika;
  11. Kufanya utafiti wa sera, tathmini ya teknolojia, ufanisi na ufundi ili kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi; na
  12. Kuwezesha ujasiriamali na ushirikiano wa biashara katika Taasisi za utafiti.

 • Sehemu ya Sayansi na Teknolojia

  Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi na inafanya shughuli zifuatazo: -

  1. Kutengeneza na kuhakiki sera, sheria na kanuni zinazohusiana na Sayansi, Teknolojia, Ubunifu, Maendeleo na Uhawilishaji na kufuatilia utekelezaji wake;
  2. Kuhamasisha uanzishwaji wa mfumo wa kisheria na udhibiti juu ya maendeleo na uwahilishaji wa Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu;
  3. Kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya utafutaji masoko na uuzaji wa matokeo ya utafiti, teknolojia ubunifu na ugunduzi;
  4. Kusimamia ulinzi wa Ubunifu, Ugunduzi na Hakimiliki za Miliki Dhihini nchini;
  5. Kuwezesha na kuratibu uanzishwaji wa Hifadhi za Sayansi, vituo vipya vya ubora katika sayansi na teknolojia na kusimamia ufanisi wao nchini;
  6. Kutambua na kuanzisha utaratibu wa kuhamasisha upatikanaji na matumizi ya teknolojia zifaazo;
  7. Kuwezesha uhawilishaji na matumizi ya teknolojia zinazofaa kwa umma kwa maendeleo ya kiuchumi;
  8. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mipango na miongozo ya maendeleo ya wabunifu / wawekezaji nchini;
  9. Kuwezesha ukuzwaji wa ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa katika utafiti na maendeleo, sayansi, teknolojia na ubunifu;
  10. Kuwezesha ubia na ushirikiano kati ya sekta ya umma, sekta ya taaluma na binafsi katika maendeleo ya sayansi teknolojia na ubunifu;
  11. Kuwezesha uendelezaji wa rasilimali watu katika sayansi, teknolojia na ubunifu;
  12. Kuwezesha kuimarishwa kwa masuala ya jinsia katika mipango ya sayansi, teknolojia na ubunifu; na
  13. Kusimamia uanzishwaji na matumizi ya Mfuko wa Ubunifu.

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce  Ndalichako akisaini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano  katika Sekta ya Elimu Kati ya Tanzania na Hungary, mjini Budapest nchini Hungary.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce  Ndalichako amesaini  mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano  katika Sekta ya Elimu Kati ya Tanzania na Hungary, mjini Budapest nchini Hungary.
Kurasa 1 ya 24

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…