Sayansi Teknolojia na Ubunifu
Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi na ina sehemu mbili (2) zifuatazo: -
- Sehemu ya Utafiti na Maendeleo; na
- Sehemu ya Sayansi na Teknolojia.
Lengo
Kutoa sera na miongozo juu ya utafiti na maendeleo, na ubunifu likiwa na lengo la kuibadilisha nchi kuwa yenye jamii iliyoelimika.
Majukumu
- Kuandaa, kurekebisha na kufuatilia utekelezaji wa sera, miongozo na viwango husika vya sayansi, teknolojia, na ubunifu;
- Kuhamasisha ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia nchini;
- Kuweka mazingira mazuri ya kiutafiti kuhusu sayansi, teknolojia na ubunifu nchini;
- Kuwaandaa wafanyakazi wenye uweledi juu ya sayansi na teknolojia kulingana na wizara / sekta husika;
- Kuanzisha na kusimamia taasisi za sayansi na teknolojia nchini;
- Kuunda na kuratibu utekelezaji wa mfumo wa ubunifu wa kitaifa;
- Kuhamasisha tasnia na sekta binafsi ili kuongeza uwekezaji wake katika maendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu;
- Kuanzisha na kusimamia utendaji wa mfuko wa Taifa wa Utafiti.
Sehemu ya Utafiti na Maendeleo
Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi, na inafanya shughuli zifuatazo: -
- Kuandaa na kuhakiki sera ya taifa ya utafiti na kufuatilia utekelezaji wake;
- Kuhamasisha maendeleo ya ujuzi wa utafiti na rasilimali watu katika utafiti;
- Kuhamasisha matumizi sahihi ya rasilimali za utafiti kupitia mipango ya kitaasisi ya kimkakati, ushirikiano kati ya taasisi na sekta husika;
- Kuwezesha shughuli za utafiti wa kiushindani zinazohusiana na tasnia na sekta binafsi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi;
- Kuanzisha na kuratibu maendeleo ya Masuala ya Utafiti ya Taifa (NRA);
- Kuendeleza na kuratibu mkakati wa utafiti na maendeleo, halikadhalika usambazaji wa matokeo ya utafiti na matumizi yake;
- Kuwezesha uanzishwaji na kusimamia uongozi wa mfuko wa utafiti wa kitaifa;
- Kujenga mazingira na mfumo bora wa ushiriki wa sekta binafsi katika utafiti;
- Kuendeleza utaratibu wa kukuza ushirikiano katika utafiti kati ya taasisi mbalimbali;
- Kuhamasisha ushirikiano kati ya sekta na biashara ili kutambua mahitaji na rasilimali za sekta hizi na kufafanua mipango ya utafiti husika;
- Kufanya utafiti wa sera, tathmini ya teknolojia, ufanisi na ufundi ili kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi; na
- Kuwezesha ujasiriamali na ushirikiano wa biashara katika Taasisi za utafiti.
Sehemu ya Sayansi na Teknolojia
Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi na inafanya shughuli zifuatazo: -
- Kutengeneza na kuhakiki sera, sheria na kanuni zinazohusiana na Sayansi, Teknolojia, Ubunifu, Maendeleo na Uhawilishaji na kufuatilia utekelezaji wake;
- Kuhamasisha uanzishwaji wa mfumo wa kisheria na udhibiti juu ya maendeleo na uwahilishaji wa Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu;
- Kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya utafutaji masoko na uuzaji wa matokeo ya utafiti, teknolojia ubunifu na ugunduzi;
- Kusimamia ulinzi wa Ubunifu, Ugunduzi na Hakimiliki za Miliki Dhihini nchini;
- Kuwezesha na kuratibu uanzishwaji wa Hifadhi za Sayansi, vituo vipya vya ubora katika sayansi na teknolojia na kusimamia ufanisi wao nchini;
- Kutambua na kuanzisha utaratibu wa kuhamasisha upatikanaji na matumizi ya teknolojia zifaazo;
- Kuwezesha uhawilishaji na matumizi ya teknolojia zinazofaa kwa umma kwa maendeleo ya kiuchumi;
- Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mipango na miongozo ya maendeleo ya wabunifu / wawekezaji nchini;
- Kuwezesha ukuzwaji wa ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa katika utafiti na maendeleo, sayansi, teknolojia na ubunifu;
- Kuwezesha ubia na ushirikiano kati ya sekta ya umma, sekta ya taaluma na binafsi katika maendeleo ya sayansi teknolojia na ubunifu;
- Kuwezesha uendelezaji wa rasilimali watu katika sayansi, teknolojia na ubunifu;
- Kuwezesha kuimarishwa kwa masuala ya jinsia katika mipango ya sayansi, teknolojia na ubunifu; na
- Kusimamia uanzishwaji na matumizi ya Mfuko wa Ubunifu.