Jumanne, 22 Septemba 2020 23:35

TANZANIA NA UJERUMANI KUENDELEZA USHIRIKIANO KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU

Serikalini ya Tanzania na Ujerumani wamekubalina kuendeleza mashirikiano kwenye elimu ya juu, Ufundi na Msingi ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata ujuzi wa kuweza kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wawakilishi kutoka ubalozi wa Ujerumani na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kilichofanyika katika Ofisi za wizara Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Dkt Leonard Akwilapo amesema kwa sasa nchi inatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi hivyo kuna uhitaji wa wataalamu wenye ujuzi katika eneo.

“Tunajenga reli ya kisasa ya umeme SGR, madaraja na ipo miradi mingine mikubwa inatekelezwa, pamoja na kwamba tunao wataalamu wetu nchini bado tunahitaji wajiendeleze ili kupata ujuzi zaidi. Kwa hiyo tumezungumza nao kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kuwezesha mafunzo kwa Vijana hapa nchini na hata nchini kwao,” aliongeza Dkt. Akwilapo.

Akizungumzia uimarishaji wa elimu ya Msingi Katibu Mkuu Akwilapo amesema wamekubaliana kushirikiana kuongeza ujuzi wa walimu katika mbinu mpya za ufundishaji ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya kufundishia.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Maendeleo katika Ubalozi wa Ujerumani nchini Dkt. Katrin Bornemann amesema Serikali ya Ujerumani itaendeleza ushirikiano wa muda mrefu ambao wamekuwa nao katika elimu ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanaendelea kupata Elimu bora.

Ushirikiano wa Tanzania na Ujerumani ni wa muda mrefu kuanzia miaka ya 80 na 90 ambapo kupitia shirika lake la DAAD waliweza kutoa ufadhili wa masomo kwa wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Read 1655 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…