Jumanne, 25 Agosti 2020 20:19

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI MWAKA WA MASOMO 2020/2021

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari. Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha NNE na SITA wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

 

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III . Waombaji wa Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02) za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari kidato cha I-IV. Aidha kwa waombaji ambao moja ya “Principal Pass”mbili ni somo la Uchumi  “Economics”, wanaweza kuomba kozi za fani ambazo ni  Michezo (Physical Education and sports), Muziki, Sanaa za Ufundi (Fine Arts), na Sanaa za Maonesho (Theatre and Performing Arts).

AINA YA MAFUNZO NA SIFA

Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo

A.   MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

Na. AINA YA MAFUNZO SIFA ZA KUJIUNGA VYUO MUDA WA MAFUNZO
1

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi

 1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati,English na Sayansi.
 2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

Bustani TC, Ilonga TC, Kabanga TC, Katoke TC

Kitangali TC, Kinampanda TC, Mandaka TC

Mtwara (U) TC, Mhonda TC, Murutunguru TC

Mpuguso TC, Singachini TC,

Tandala TC, Tarime TC Vikindu TC, Nachingwea TC, Ndala TC, Mamire TC, Shinyanga TC, Marangu TC, na Dakawa TC

Miaka 3

2

Stashahada  ya Ualimu Elimu Maalum

 1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati na Sayansi
 2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.
Patandi TC

Miaka 3

3

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali

 1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III   Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza.
 2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

Kinampanda TC, Nachingwea TC, Mhonda TC

Tarime TC, Vikindu TC, Mpuguso TC, Mandaka TC,  Singachini TC

Murutunguru TC, Kabanga TC, Bustani TC

Ndala TC, Katoke TC, Bunda TC, Tarime TC

Miaka 3

4

Stashahada ya Ualimu Elimu kwa Michezo 

 1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya sayansi na hisabati.
 2. Aliyehitimu Kidato cha VI au uzoefu katika michezo ni sifa ya nyongeza.                               

Tarime TC, Mtwara (K) TC, Ilonga TC

                                          

Miaka 3

5 Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (English Medium)
 1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu somo la English
 2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.                               

Dakawa TC, Marangu TC

                                          

Miaka 3

B.    MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI

1

Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati

Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili katika masomo ya Tahasusi za Sayansi, Hisabati na TEHAMA kwa kuzingatia Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kama ifuatavyo: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agriculture Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science.

Mamire TC, Monduli TC, Mandaka TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC

Miaka 2

2

Stashahada ya Sayansi ya Jamii, Biashara  na Lugha

Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili kwa kuzingatia masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari Kidato cha I-IV. Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kidato cha I-IV ni : Kiswahili, English, History, Geography, Civics, Commerce and Book keeping.

Bunda TC, Mtwara (K) TC,

Marangu TC, Nachingwea TC, Shinyanga TC, Mandaka TC, Mpuguso TC, Dakawa TC,  Butimba TC, Tabora TC,

Morogoro TC, Tarime TC, Shinyanga TC,

Miaka 2

3 Stashahada ya Ualimu Michezo, Muziki, Sanaa za Ufundi na Sanaa za Maonesho

Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili pamoja na ufaulu wa masomo ya liyoainishwa katika mtihani wa kidato cha IV kwa kila kozi kama ifuatavyo:

Butimba TC

Miaka 2

(a)    Sanaa za Ufundi: masomo ya Fine Arts, Basic Mathematics, Chemistry, History, Physics, English na Civil Engineering. Butimba TC

Miaka 2

(b)   Sanaa za Maonesho: masomo ya English, Literature in English, Kiswahili, Geography na History. Butimba  TC

Miaka 2

(c)  Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na masomo ya English, Kiswahili, Physics, Geography, History na Biology. Butimba TC

Miaka 2

(d)  Elimu kwa Michezo: masomo ya Physical Education and sports, Languages, na Biology. Butimba TC na Mtwara (K)

Miaka 2

C.     MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (STASHAHADA ELIMU MSINGI NA STASHAHADA ELIMU SEKONDARI)

Na.

AINA YA MAFUNZO SIFA ZA KUJIUNGA CHUO MUDA WA MAFUNZO

1

Stashahada Elimu Maalum (Mafunzo kazini) Msingi Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Astashahada, Stashahada au Shahada kwa ufaulu wa angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Nne na awe na uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka miwili (2) Patandi TC Miaka 2

2

Stashahada Elimu Maalum (Mafunzo Kazini) Sekondari

Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada, Stashahada ya Elimu ya Juu au Shahada mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka 2; na

Aliyefaulu masomo ya Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Sita

Patandi TC Miaka 2

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

 1. Tangazo hili halitawahusu wahitimu wa kidato cha Nne 2019 waliochaguliwa kujiunga na  Mafunzo ya Ualimu 2020/2021 kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI . Aidha wahitimu wengine waliohitimu kuanzia 2017 hadi sasa wanaruhusiwa kutuma maombi.
 2. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kielektroniki kupitia tovuti (https://tcm.moe.go.tz , au BOFYA HAPA KUJISAJILI/KUINGIA KWENYE MFUMO WA MAOMBI YA UALIMU)
 3. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika Chuo anachotaka kusoma na Vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki.
 4. Waombaji  wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali watachagua tahasusi hadi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi.
 5. Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada au Shahada.
 6. Walimu Kazini watapaswa kuambatisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao;
 7. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.
 8. Fomu  za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz , au BOFYA HAPA KUPATA FOMU) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
 9. Mwisho wa kutuma maombi kwa Mafunzo ya Ualimu  ni tarehe 15/09/2020.
TANBIHI:
 • Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu. 
 • Majibu ya maombi yatapatikana kupitia akaunti ambayo mwombaji aliitumia kufanya maombi.
 • Mwombaji atabofya mahali palipoandikwa HALI YA MAJIBU ili kuona chuo alichochaguliwa.
 •  Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii 0620-198-019 au 0752-480-999
Read 57722 times

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…