Jumatano, 01 Julai 2020 17:05

NDALICHAKO ATIMIZA AHADI ATOA CHEREHANI 10 VETA MPANDA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo Julai 1, 2020 ametimiza ahadi ya kutoa cherehani 10 kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Mpanda? wanaotoka katika mazingira magumu waliohitimu mafunzo ya ushonaji.

Akizungumza katika halfa ya utoaji wa cherehani hizo Mkoani Katavi, Profesa Ndalichako amesema ahadi hiyo alitoa? mwaka 2018 baada ya kuwakuta vijana wadogo wamemaliza masomo ya darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari waliamua kujiunga na mafunzo ya ushonaji katika chuo hicho kupitia ufadhili wa kanisa.
?
“Mwaka juzi nilifika katika chuo hiki niliwakuta hawa vijana wawili wadogo wakiwa katika mafunzo ya ushonaji na nilipozungumza nao niligundua kuwa ni wadogo, lakini pia wametoka katika mazingira magumu, hivyo kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari ndipo nilipowaahidi kuwapatia cherehani watakapomaliza ili ziwawezeshe kujiajiri, lakini nimetoa 10 ili na wengine wenye mazingira ya namna hiyo wapate ” amesema Waziri Ndalichako.

Aidha, Waziri huyo amenuagiza Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Mpanda kuona namna ya kuwapatia nafasi ya kuendelea na ngazi nyingine ya mafunzo watoto hao ili kuwawezesha kuwa mahiri katika ushonaji na kuhakikisha anawasimamia na kuwashauri popote watakapokuwa wanafanya shughuli zao.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Mpanda Elisha amemshukuru waziri kwa kutimiza ahadi aliyoitoa mwaka 2018 kwani inakwenda kuinua watoto wanaotoka katika familia masikini, na kuahidi kuendelea kuwasimamia ili cherehani hizo ziwe na manufaa kwa watoto webyewe na familia zao.

Mmoja wa wanafunzi waliopatiwa cherehani Gift Giles amemshukuru Waziri kwa kuwapatia cherehani hizo ambazo zinakwenda kubadili maisha yao kwani zitawawezesha kupata fedha ambazo zitawasaidia kujiendeleza katika masomo

Naye .mmoja wa walezi wa wanafunzi hao bibi Flora Cosmas amemshukuru Mhe. Ndalichako na kuahidi kuwasimamia vijana wao ili wazitumie maahine hizo vizuri ikiwa ni pamoja na kuwaendeleza zaìdi kiujuzi wanafunzi hao.

"Sisi walezi wa vijana hawa tunamahukuru sana Mhe. Waziri kwa kuguswa kwake kuamua kwa moyo wake kufanya jambo hili kubwa maana anakwenda badili naisha ya vijana hawa ambao hawakuwa na uwezo wa kununua hizi cherehani" amesema bi Cosmas.

Waziri Ndalichako alikutana na wanafunzi hao na kutoa ahadi yà kuwapatia cherehani hizo alipotembelea chuo hicho mwaka 2018 na kuwakuta watoto hao wadogo wamiwa na umri wa miaka 12 na 14.

Read 2034 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…