Jumatano, 08 Aprili 2020 21:36

MKUTANO MAALUM WA KAMATI NDOGO YA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA ELIMU

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya Mkutano Maalum wa Kamati ndogo ya Baraza la Wafanyakazi kwa lengo la kujadili makadirio ya Bajeti ya mwaka 2020/21.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Leornad Akwilapo amesema Baraza hilo ambalo ni maalum la wafanyakazi limefanyika kwa kuhudhuriwa na wajumbe wachache kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Corona.

Ameongeza kuwa pamoja na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka 2020/21, mkutano huo pia umejadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2019/20.

"Tumekutana katika mkutano huu maalum kwa sababu ya kanuni na sheria ambayo inataka baraza kukaa kupitia bajeti ya Wizara kabla ya kuwasilishwa Bungeni," amesema Dkt. Akwilapo.

Aidha, amewashukuru viongozi na watumishi wa Wizara hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwataka kuongeza bidii na nguvu katika kuhakikisha malengo ya Wizara yanatekelezwa kwa ukamilifu ili kuondoa malalamiko.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Moshi Kabengwe amesema mkutano huo maalum umeitishwa kwa kufuata sheria za Baraza la wafanyakazi.
Kabengwe amesema hali ya maambukizi ya virusi ya Corona itakapotulia Wizara itaitisha Baraza kamili kwa ajili ya kuzinduliwa kutokana na kuwa na wajumbe wapya.

Aidha, Wajumbe wa mkutano huo walipata elimu juu ya maambukizi ya virusi vya Corona na namna ya kujikinga

Read 2068 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…