Jumatatu, 09 Machi 2020 16:53

WASTAAFU WATARAJIWA WIZARA YA ELIMU WAPIGWA MSASA

Jumla ya watumishi 150 wanaotarajia kustaafu utumishi wa umma katika mwaka wa fedha 2020/2021kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na wTeknolojia wamepatiwa mafunzo maalum ili kuwaandaa na maisha mapya baada ya kustaafu.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Profesa. James Mdoe amesema mafunzo hayo yanalenga kuwaelimisha na kuwakumbusha wastaafu watarajiwa kuhusu utunzaji wa afya kwa njia ya lishe bora, matumizi sahihi ya mafao na pensheni, ubunifu wa miradi, masoko na mitaji.

Profesa Mdoe amewaasa watumishi hao kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini ili yaweze kuwasaidi baada ya kustaafu.

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Moshi Kabengwe amesema miongoni mwa mafunzo watakayopatiwa watumishi hao ni pamoja na dhana ya kustaafu Utumishi wa Umma, Umuhimu wa kupanga mapema Mipango ya maisha kabla ya kuondoka kwenye Utumishi wa Umma na fursa za kujipatia kipato zilizopo katika soko.

Mafunzo mengine ni vyanzo vya upatikanaji mitaji, upatikanaji wa masoko, Mbinu za kuboresha afya ili kuendelea kuwa na afya bora na mbinu za kuepuka misongo na changamoto za kimaisha.

Read 2064 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…