Jumamosi, 02 Novemba 2019 11:50

WAZIRI WA ELIMU AZIAGIZA TAASISI ZOTE ZA ELIMU KUANZISHA MICHEZO KWA WATUMISHI WAKE.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameziagiza taasisi zote za elimu kuazisha michezo kwa watumishi wake ili kuimarisha afya ya mwili.

Profesa Ndalichako ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati wa kufunga mashindano ya michezo mbalimbali ya Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) ambapo amesema afya ya mwili inapoimarika hata afya ya akili nayo inaimarika

"Watu wanasema michezo ni afya, ni ajira na furaha hivyo tuhakikishe tunaimarisha afya na kupata ajira kupitia kwenye michezo" amesema Profesa Ndalichako

Waziri Ndalichako amesema taifa linahitaji nguvu kazi yenye nguvu na afya bora na kati ya mambo yanayoboresha afya ni pamoja na michezo na mazoezi

Amesema serikali ya awamu ya tano inaimiza suala la michezo na kutenga kila Jumamosi ya pili ya mwezi kuwa ni siku ya michezo na mazoezi , huku ikiwekeza katika michezo na sasa tunashuhudia hata timu za taifa zikishiriki vizuri katika mashindano ya kimataifa

Akizungumza katika mashindano hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Profesa..... Chibunda amesema katika kipindi cha miaka 10 shughuli za michezo katika Chuo hicho iliteteleka kutokana na sababu mbalimbali na mwaka 2017 zimeanza tena baada ya kupata ufadhili wa Benki ya CRDB.

Read 1254 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…