Print this page
Ijumaa, 01 Novemba 2019 11:04

ZIARA YA MH. WAZIRI SHULE YA SEKONDARI YA KILIMO KILOSA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo Novemba 1, 2019 amefanya ziara katika shule ya sekondari ya Kilimo Kilosa kukagua utekelezaji wa ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.

Waziri Ndalichako pamoja na kukagua ukarabati wa miumdombinu ya shule hiyo pia ametoa mashine ya kudurufu (photocopy mashine) kwa shule hiyo itakayosaidia katika kufundishia na kujifunzia na shughuli za utawala.

Akiwa katika ziara hiyo Profesa Ndalichako amesema zawadi hiyo ameitoa kufuatia ombi lilotolewa kwake mmoja wa wahitimu wa Shule hiyo Ndugu Bashiru Ally ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.

" nampongeza Dkt. Bashiru ambae amekuwa akirudi mara kwa mara kushiriki kuchangia maendeleo ya shule hii aliyosoma na leo nimeleta mashine aliyoomba kwa ajili yenu".

Katika ziara hiyo Ndalichako pia amempongeza Mkuu wa Wilaya na Halmashauri kwa kusimamia vema ukarabati ambao unafanyika kwa ubora na kwa wakati na kwa kutumia vema rasilimali fedha zilizoletwa kwa ajili ya ukarabati huo.

" shule hii ililetewa shilingi Milioni 754 lakini katika kutekeleza wametumia shilingi milioni 602 tu. Hakika mnastahili pongezi kwa ubora wa kazi lakini na chenji imebaki".

Kufuatia hatua hiyo Ndalichako ameagiza fedha zinazobaki zaidi ya Shilingi Milioni 100 zitumike kukarabati nyumba za walimu katika shule hiyo.

Shule hiyo inafanyiwa ukarabati ikiwa ni kuendelea na utekelezaji wa mpango wa ukarabati wa shule kongwe 88 unaotekelezwa na serikali

Ukarabati wa shule hiyo unafanywa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kwa gharama ya shilingi milioni 754 unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 15. Novemba na tayari ukarabati umefikia asilimia 75.

Mkuu wa Wilya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi amesema wilaya yake imejipanga katika kuhakikisha kaxi hiyo inakamilika kwq ubora w a hali ya juu ili kurejesha shule hiyo katika hali yake ya awali. Amemahukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kipaumbele katika miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ya Elimu na kipekee kwa mradi huo wa ukarabati wa shule katika WIlaya hiyo ikiwemo Shule hiyo ya Sekondari ya Kilimo ya Kilosa na Shule ya Sekondari Dakawa.

" tunashukuru sana Serikali kwa uwekezaji huu mkubwa katika kukarabati shule hizi, pamoja na mafundi wetu wanaotekeleza mradi huu ambapo tutumia force account".

Nae Mkuu wa shule hiyo ameahidi kuwa kufuatia ukarabati huo wanafunzi watakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia na hivyo matarajio ni kuongeza ufaulu katika mitihani ya kitaifa.

Read 1328 times
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…