Jumamosi, 05 Oktoba 2019 21:39

WIZARA YA ELIMU YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujengeana ufahamu wa kile Wizara inachotekeleza lakini pia ni kuendeleza mahusiano mazuri ya kiutendaji baina ya Wizara na Vyombo vya Habari nchini.

Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo amesema Wizara inatambua kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya habari nchini ya kuhabarisha na kuelimisha hivyo mkutano huu ni chachu ya kuendeleza mahusioano katika utendaji kazi na vyombo vya habari.

“Kwa kweli ninyi wahariri mmekuwa wachambuzi wazuri katika kuhakikisha mnato yale ambayo kama wizara yanatuweka katika nafasi nzuri kwa kuchakata, kuchapisha habari na taarifa mbalimbali kwa lengo la kuhabarisha na kuelimisha kile kinachotekelezwa na sekta ya elimu”amesema Dkt. Akwilapo

Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara hiyo Sylvia Lupembe amesema kufanyika kwa mkutano huo ni utekelezaji wa Mkakati wa Wizara ambao umejiwekea wa kuhakisha tunaendeleza mahusiano mazuri na vyombo vya habari ili kuhakikisha habari mbalimbali za Sekta ya Elimu zinasikia kwa wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya wahariri waliohudhuria mkutano huyo Mhariri wa Habari kutoka Clouds Media Joyce Shebe ameishukuru Wizara kwa kuona umuhimu wa kufanya Mkutano na vyombo vya habari kwa kuwa unawajengea uelewa wa kile Sekta ya Elimu inachotekeleza na kuwawezesha kundika habari kwa usahihi.

Aidha Shebe amesema wako tayari kushirikiana na Wizara katika kutoa habari za kuhamasisha umuhimu wa Elimu lakini pia kazi nzuri zinazofanywa na Sekta ya Elimu katika maeneo pembezoni.

Mkutano huo umehudhuriwa naWahariri wa Vyombo vya Habari nchini pamoja na baadhi ya wakurugenzi na Waratibu wa Miradi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambao wamepata fursa ya kuelezea kwa wahariri kile wanachotekeleza katika maeneo wanayosimamia.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
5/10/2019

Read 1575 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…