Ijumaa, 02 Agosti 2019 14:50

WIZARA YA ELIMU KUSIMAMIA, KUBAINI NA KUKUZA WABUNIFU CHIPUKIZI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali inatambua umuhimu wa Sayansi Teknolojia na Ubunifu ktk maendeleo ya taifa letu na hivyo itaendelea kusimamia na kuendeleza wanasayansi wabunifu nchini.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya tisa ya wanasayansi watafiti chipukizi nchini yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania, (YST) jijini Dar Es Salaam

Maonesho hayo huwahusisha wanasayansi wanafunzi kutoka shule za sekondari kote nchini , kuonesha tafiti walizofanya kupitia mpango wa YST.

Ndalichako amewapongeza wanafunzi walioshiriki kwa kuonesha tafiti zilizofanywa kisayansi na ubora na pia kwa kutumia teknolojia katika kubuni mambo mbalimbali na mifumo inayotoa utatuzi wa changamoto za jamii yetu.

Amepongeza walimu wanaoshiriki katika mpango huo kwa kuweza kutoa hamasa kwa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na hisabati na kwa kufundisha vizuri hali ambayo inajionesha kupitia kazi bora za wanafunzi wao.

Read 1600 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…