Jumatatu, 29 Aprili 2019 15:41

WAZIRI NDALICHAKO AIPONGEZA CHINA KWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameipongeza Jamhuri ya Watu wa China kwa kuimarisha ushirikiano  na  Tanzania hususan katika sekta za Elimu,

Biashara na Ujenzi wa miundombinu.

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo wakati wa sherehe za kuhadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa Kideplomasia kati ya Tanzania na China ambapo amesema kuwa mahusiano kati ya nchi hizo mbili ni ya muda mrefu.

Aidha, Prof. Ndalichako amesema mchango wa nchi hiyo kwenye maendeleo ya Tanzania ni dhahiri akitolea mfano  wa ujenzi wa Reli ya TAZARA pamoja na ujenzi wa viwanda mbalimbali vya nguo nchini.

Prof. Ndalichako amesema pia China imeendelea kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa kubadilishana uzoefu

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda, Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara, na viongozi mbalimbali kutoka Taasisi  za umma na binafsi nchini. 

Read 1525 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…