Jumatano, 05 Desemba 2018 08:40

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASISITIZA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA SEKTA YA ELIMU

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ikitumika vizuri katika sekta ya elimu itasaidia kujenga mazingira mazuri na kuwezesha kuwepo kwa mbinu bora katika ufundishaji na ujifunzaji.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo jijini Dar Es Salaam katika halfa ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa mashindano ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa mwaka 2018 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Huawei Tanzania, na kusisitiza kuwa kutumia TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji Mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wengi waliosehemu tofauti.

Mhe. Majaliwa amewataka wanafunzi kutumia fursa ya mashindano hayo kuendelea kujifunza TEHAMA ili wewe na uwezo wa kumiliki mifumo ambayo itasaidia nchi katika kurahisisha utendaji wa shughuli zake kupitia sayansi na Teknolojia

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inaendelea kuunganisha mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye taasisi zake ili kufanikisha azma ya serikali ya kurahisisha utendaji kazi.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Elimu, Sayansi naTeknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka vijana walioshiriki katika mashindano hayo kuendelea kujifunza zaidi kwani nchi bado inahitaji Maendeleo katika kipindi ambacho serikali imekusudia kujenga uchumi wa viwanda.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa HUAWEI Tanzania Frank Zhou amesema kabla ya vijana hao kuingia katika mashindano hayo walipatiwa mafunzo ili kuwawezesha kuzitambua Teknolojia za kisasa kwa kuwa Teknolojia inakua kila siku.

Mashindano hayo ya TEHAMA yalianza na vijana 500 lakini mpaka mwishoni vijana 10 tu ndio wamefanikiwa kushinda ambapo washindi watatu wa juu wanatarajiwa kwenda katika nchi za Afrika Kusini na China kwa lengo la kujifunza zaidi masuala ya TEHAMA.

Imetolewa na:

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

05/12/2018

Read 675 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…