Ijumaa, 02 Novemba 2018 08:31

SERIKALI KUTOA MWONGOZO WA USAMBAZAJI KOMPYUTA SHULENI

Serikali imesema inatarajia kutoa mwongozo wa utaratibu wa kusambaza kompyuta na vifaa vyake katika shule za msingi na sekondari ili kuwezesha vifaa hivyo kutambuliwa ikiwa ni pamoja na kuwa na takwimu sahihi kwa shule ambazo zitakuwa zimepatiwa vifaa hivyo.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya TEHAMA yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo amesema kwa sasa ni vigumu kwa serikali kujua ni shule ngapi zenye kompyuta ama taasisi zinazotoa misaada ya kompyuta shuleni.

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakaa pamoja na Ofisi ya Rais Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa ili tuweze kuweka mwongozo ambao utawezesha serikali kutambua taasisi zote zinazojishughulisha na usambazaji wa kompyu takatika shule pamoja na kutambua shule zilizo na kompyuta ili iwe rahisi kuziratibu”amesema Prof. Mdoe.

Akizungumza na Walimu walioshiriki mafunzo hayo amewataka kuhakikisha wanatumia maarifa waliyoyapata katika kuboresha elimu na kuimarisha utendaji wa kazi ili kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Pius Joseph amesema mfuko wa Mawasiliano kwa wote ina jukumu la kuhakikisha ina ziunganisha shule zote za msingi na sekondari katika mtandao wa inteneti, pamoja na kutoa vifaa na mafunzo kwa walimu wanaofundisha masomo ya TEHAMA .

Mfuko huo wa Mawasiliano tayari umetoa mafunzo yaTEHAMA kwa walimu 578 kutoka mikoa yote ya Tanzania pia umetoa kompyuta 425 kwa shule za msingi, komputa 1250 kwa shule za sekondari na kuwa vifaa hivyo vimetolewa katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018.

Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

02/11/2018

Read 673 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…