Jumanne, 30 Oktoba 2018 09:23

PROF NDALICHAKO: TATUENI CHANGAMOTO ZENU KIMIFUMO

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewashauri watumishi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto za mikopo ya Wanafunzi kwa njia ya mifumo.

Waziri Ndalichako amesema hayo jijini Dar Es Salaam alipotembelea ofisi ya HESLB lengo la kujiridhisha na hali ya mwenendo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2018/2019.

Katika ziara hiyo licha ya kukutana na Menejimenti ya HESLB, Prof. Ndalichako pia aliongea na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Profesa Charles Kihampa kuhusu hali ya udahili wa Wanafunzi wa Elimu ya juu ambapo Kihampa alitumia nafasi hiyo pia kukabidhi orodha ya Wanafunzi 2,600 ambao udahili wao umethibitishwa.

Awali katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru ilisema kiasi cha shilingi bilioni 98.12 mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 27,929 kati ya wanafunzi 40,485 wa mwaka wa kwanza waliotarajiwa kupatiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

Badru alisema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 12,556 watapangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 42 katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyokusudiwa.

Aliongeza kuwa idadi ya wanafunzi 27,929 waliokwishapangiwa mikopo na ambao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vinavyotambulika ni asilimia 69 ya wanafunzi 40,485 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

Orodha ya majina ya wanafunzi hao  27,929 (Awamu ya kwanza 25,532 na awamu ya pili 2,397) waliokwishapangiwa mikopo inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo hiyo.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NATEKNOLOJI

30/10/2018

Read 224 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…