Jumanne, 04 Septemba 2018 11:19

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA CHUO CHA UALIMU MURUTUNGURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Magufuli leo ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya upanuzi wa Chuo Cha Ualimu Murutunguru,

kilichopo Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Rais Magufuli amesema Chuo Cha Murutunguru kwa sasa walimu wanaohitimu ni ngazi ya cheti, lengo la serikali ni kianze kutoa ngazi ya Diploma na baadae kikiongezewa miundombinu kiweze kutoa shahada.

Rais Magfuli pia amewapongeza Viongozi wa Wizara ya Elimu kwa kusimamia vizuri miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo.

Pia Rais amewashukuru  washirika wa Maendeleo hususan nchi ya Uingereza kwa kuendelea kufadhili miradi ya Elimu.

Upanuzi wa ujenzi wa Chuo hicho unahusisha jengo la Utawala, vyumba vya madarasa, bwalo la Chakula, hosteli za wanafunzi, jengo maalumu la kupokelea umeme na ujenzi wa mifumo ya Maji na umeme.

Ujenzi huo utagharimu takriban bilioni mbili nukta Tatu na inatarajia kukamilika oktoba mwaka huu.

Imetolewa na;

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
4/9/2018
Read 502 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…