Ijumaa, 31 Agosti 2018 12:26

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU AWATAKA WAKUU WA VYUO VYA UALIMU KUFUATA TARATIBU KATIKA UTENDAJI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo amewataka Wakuu wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafuate taratibu

wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi ikiwa ni pamoja na kushirikisha watumishi na wanafunzi wa Chuo taarifa za mapato na matumizi ya fedha.

Dk. Akwilapo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati alipokutana na Wakuuu wa Vyuo hivyo kwa lengo la kujadili mafanikio, changamoto na mikakati waliyonayo katika kuhakikisha majukumu na uendeshaji wa vyuo yanatekelezeka bila changamoto ili waweze kufikia azma ya kuandaa walimu bora.

Pia Katibu Mkuu huyo amewataka Wakuu wa Vyuo kuwasirikisha wale wanaowasimamia katika kuandaa mikakati ya utendaji ili waweze kutoa mchango katika kutekeleza mikakati hiyo na kufikia malengo mapana ya Wizara ambayo ni kutoa Elimu bora

Katika hatua nyingine Dk. Akwilapo amewataka Wakuu wa Vyuo hao kuanisha mahitaji ya rasilimali watu ambayo inahitajika vyuoni inayoendana na kozi zinazofundishwa katika Chuo husika ili kuepuka kuwa na rasilimaliwatu isiyoendana na mahitaji ya Chuo.

Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu Morogoro Agustine Sahili amesema wanaishukuru Wizara kwa kuandaa vikao vya aina hiyo kwani vinawasaidia kuwakumbishia taratibu za kazi na kuahidi kutekeleza yale yote waliyoagizwa ili kuimarisha utendaji katika maeneo ya kazi.

Kikao kazi hicho kimeshirikisha Wakuu wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali 35 vilivyopo hapa nchini.

Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
31/08/2018
Read 782 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…