Jumatano, 06 Juni 2018 09:52

OLE NASHA: SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA DFID

Serikali imehaidi kuendelea kushirikiana na wadau wa Sekta ya Elimu katika kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata Elimu iliyo bora ili kufikia malengo ya mkakati wa kuwa na uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Wiliam Ole Nasha jijini Dar es Salaam katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha Wadau wa Elimu walio chini ya Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza-DFID

Naibu Waziri Ole Nasha amesema ushirikiano wa serikali ambao umekuwepo kwa muda mrefu na wadau hao wa Elimu DFID umechangia katika kuhakikisha mtoto wa Kitanzania anapata Elimu iliyobora.

“Elimu bora kwa kila mtoto wa kitanzania ndiyo msimamo wa Serikali, katika kutekeleza hilo sera ya Elimu bila malipo imekuwa na baadhi ya chagamoto na katika kukabiliana nazo ndiyo maana wamekuwepo wadau wa Elimu ambapo sasa wanafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kutimiza malengo yanayokusudiwa, kwani hatuwezi kuboresha Elimu kama kila mtu atafanya kazi peke yake, Umoja ni Nguvu.”amesema Mheshimiwa Ole Nasha.

Ole Nasha amesema mpaka sasa wadau hao wa Elimu kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) wameshatoa kiasi cha zaidi ya bilioni 200 ambazo zimekusudiwa kufanya uboreshaji wa Miundombinu ya shule za msingi na Sekondari, pamoja na kukarabati na kujenga vyuo vya Ualimu.

Naye Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza-DFID Jane Miller ameishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata katika kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika kama zilivyokusdiwa.Kikao hicho kimewashirikisha wadau wa Elimu kutoka EQUIP –T, EP4R,HDIF,GPE, British Council, GPE, na RISE

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serialini

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Read 741 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…