Jumamosi, 26 Mai 2018 09:14

ZAIDI YA BILIONI NNE KUTUMIKA KWENYE MIRADI YA UTAFITI. WAZIRI NDALICHAKO ASISITIZA KUWA ZISITUMIKE VINGINEVYO

Serikali imetoa zaidi ya bilioni nne kwa ajili ya Taasisi na Watafiti walioshinda maandiko ya miradi 8 ya utafiti ambayo itaanza kufadhiliwa mwaka huu wa fedha.

 

Akizungumza jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhi hundi kwa Taasisi zilizoshinda fedha hizo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amesema miradi yote iliyopata fedha ni ile ambayo ina malengo madhubuti ya kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo 2025.

Waziri Ndalichako amesema kufadhiliwa kwa miradi hiyo nane kutaleta mchango mkubwa wa uzalishaji wa dawa nchini na kupunguza uagizwaji wa dawa kutoka nje, uboreshaji wa maabara za uhandishi jeni, kuongeza ushindani wa bidhaa, kuongeza uzalishaji wa mazao, uzalishaji wa mimea, pamoja na kuchangia katika uanzishwaji wa viwanda.

Waziri Ndalichako amezitaka taasisi zilizopata fedha hizo kuzitumia kwa uadilifu na kwa malengo yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo.

Miradi hiyo nane ni pamoja na ule wa umaliziaji wa kiwanda cha uzalishaji wa dawa na maabara ya utafiti ya mabibo, uimarishaji wa miundombinu ya utafiti na ugunduzi wa dawa katika chuo kikuu cha tiba (MUHAS), Muhimbili, ununuzi wa vifaa na uboreshaji wa maabara ya uhandisi jeni ya Taasisi ya Mifugo TALIRI kwa ajili ya kuongeza kasi ya uzalishaji wa mifugo, Uboreshaji wa maabara ya Chanjo ya Taasisi ya Taifa Kibaha.

Miradi mingine ni Uboreshaji wa maabara ya udongo, ili kuimarisha Afya ya Udongo kwa ajili ya kilimo endelevu kwa lengo la kuimarisha uchumi wa viwanda, Uboreshaji wa maabara ya kisasa ya utafiti wa mbogamboga na matunda kaskazini mwa Tanzania (HORTI Tengeru), Ukarabati wa mtambo wa utafiti wa kutengeneza mvinyo katika taasisi ya utafiti wa kilimo, Makutopora na uboreshaji wa usimamizi wa maabara za uchakataji wa mazao ya taasisi ya utafiti wa viwanda TIRDO.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

25/05/2018

Read 1776 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…